WATOTO WAFARIKI KWA KULA VITAFUNWA VILIVYOPIKWA KWA DAWA YA KUULIA WADUDU


Watoto wawili nchini Uganda wameaga dunia huku wengine 11 wakipelekwa hospitali baada kula kitafunwa aina ya chapati kilichotengenezwa kwa sumu ya kuua wadudu badala ya mafuta, gazeti la Daily Monitor linaripoti.

Watoto wote 13 wanatoka familia moja Budumba, magharibi mwa Uganda na  kwamba wana umri wa 5 na 6.

Gazeti hilo limeripoti kwamba watoto hao walijipikia wenyewe vitafunwa hivyo ambavyo vinafahamika kama Kabalagala.

Watoto hao inasemekana kwamba miongoni mwa viambato walivyotumia wakati wanapika ilikuwa dawa ya kuua wadudu inayonyunyizwa kwenye matikiti maji na mbogamboga zinazokuzwa wakidhani kwamba ni mafuta.

Kulingana na gazeti hilo, watoto hao walianza kutapika na kupelekwa hospitali ya Busolwe ambapo wawili wao waliaga dunia huku wengine 11 wakiendelea kupata matibabu.

Mkuu wa polisi wa eneo hilo, Ceasar Tusingwire alithibitisha tukio hilo.

"Watoto 13 kutoka familia moja wanashukiwa kwamba wamekula chapati zenye sumu. Walichanganya dawa ya kuua wadudu na mafuta ya kupikia kwa bahati mbaya," ameeleza bw Tusingwire.

"Walionusurika wanaendelea vizuri lakini bado hawajapa nguvu. Tunajitahidi kuhakiksha watoto wamerejea katika hali yao ya kawaida, mhudumu mmoja wa afya amesema hivyo.

Polisi imesema miili ya waliokufa inafanyiwa uchunguzi na kuongeza kwamba  upelelzi wa tukio hilo unaendelea.

Credit:BBC


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post