CHUGAZO : 'HAKUNA MWANAUME ANAKUWA JUU BILA KUSIMAMA KWENYE MABEGA YA MWANAMKE'


Mkuu wa Idara ya Ujenzi wa Nguvu za Pamoja (TAPO) TGNP Grace Kisetu akifungua warsha ya kuhusu ufuatiliaji wa kazi za uhamasishaji wa jamii juu ya umuhimu wa wanawake kushiriki katika nafasi na michakato ya maamuzi na uongozi leo Jumamosi Februari 15,2020 katika Ukumbi wa Vijana Center Mjini Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde 1 blog.
Mkuu wa Idara ya Ujenzi wa Nguvu za Pamoja (TAPO) TGNP Grace Kisetu akifungua warsha ya kuhusu ufuatiliaji wa kazi za uhamasishaji wa jamii juu ya umuhimu wa wanawake kushiriki katika nafasi na michakato ya maamuzi na uongozi iliyokutanisha pamoja imekutanisha pamoja wadau kutoka makundi ya viongozi wa mila,dini na jamii kutoka mikoa ya Shinyanga Kigoma,Tabora Mara na Simiyu.
Mkuu wa Idara ya Ujenzi wa Nguvu za Pamoja (TAPO) TGNP Grace Kisetu akifungua warsha ya kuhusu ufuatiliaji wa kazi za uhamasishaji wa jamii juu ya umuhimu wa wanawake kushiriki katika nafasi na michakato ya maamuzi na uongozi ambapo alisema lengo ni kuongeza nafasi za wanawake katika nafasi za uongozi.
Afisa Mtendaji wa kata ya Murufiti wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Cameroon Chugazo  akizungumza katika warsha hiyo. Alisema -"Hakuna kiongozi yeyote duniani ambaye anafikia mamlaka ya juu bila kusimamia mabega ya mwanamke kwa sababu mwanamke ndiye anayeandaa kiongozi wa kesho.‘Haiwezekani Orijino izae feki’,sasa kama wao wanatengeneza viongozi kwanini wao wasiwe viongozi".
Kiongozi wa Jamii Avelina Mwigulu kutoka wilaya ya Meatu mkoani Simiyu akizungumza katika warsha hiyo ambapo alisema bado kuna baadhi ya wanaume hawataki kuwaruhusu wanawake kugombea nafasi za uongozi kwa hofu ya kwamba mwanamke akiwa kiongozi atakuwa na mamlaka na nguvu zaidi kuliko mwanamke kitendo ambacho amesema siyo kweli.
Mwenyekiti wa VIKOBA kata ya Kizengi wilaya ya Uyui mkoa wa Tabora, Hobokela Joseph akizungumza katika warsha hiyo ambapo aliwataka wanawake kupuuza kauli zinazowakatisha tamaa wanawake kugombea nafasi za ,uongozi kama vile kauli za kwamba ‘Mwanamke hawezi kuwa juu ya mwanaume’, ‘mwanamke akiwa kiongozi atachukua waume za watu’ ‘mwanamke akiwa kiongozi atakuwa mhuni na malaya’,’mwanamke ni wa kuzaa tu na kulea familia’.
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa ukumbini.
Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini.
Washiriki wa warsha kutoka mkoa wa Tabora wakifanya kazi ya kikundi.
Washiriki wa warsha kutoka mkoa wa Kigoma wakifanya kazi ya kikundi.
Washiriki wa warsha kutoka mkoa wa Shinyanga wakifanya kazi ya kikundi.
Washiriki wa warsha kutoka mkoa wa Simiyu wakifanya kazi ya kikundi.
Washiriki wa warsha wakiwa nje ya ukumbi.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Wanawake wametakiwa kupuuza kauli ambazo zimekuwa zikitolewa na baadhi ya watu kuwa hawawezi kuwa viongozi kwani mwanamke ndiyo mtu pekee duniani anayeandaa watu kuwa viongozi kuanzia wakiwa watoto hivyo haiwezekani mtu anayeandaa viongozi akashindwa kuwa kiongozi.

Hayo yamesemwa leo Jumamosi Februari 15,2020 na wadau wa haki za wanawake katika Warsha ya ufuatiliaji wa kazi za uhamasishaji wa jamii juu ya umuhimu wa wanawake kushiriki katika nafasi na michakato ya maamuzi na uongozi iliyofanyika katika Ukumbi wa Vijana Center Mjini Shinyanga.

Kwa Mujibu wa Mkuu wa Idara ya Ujenzi wa Nguvu za Pamoja (TAPO) TGNP Grace Kisetu alisema warsha hiyo ya siku mbili iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) imekutanisha pamoja wadau kutoka makundi ya viongozi wa mila,dini na jamii kutoka mikoa ya Shinyanga (Kishapu),Kigoma (Kasulu), Tabora (Uyui), Mara (Tarime) na Simiyu (Meatu) kwa lengo likiwa ni kuongeza nafasi za wanawake katika nafasi za uongozi.

Akizungumza katika warsha hiyo,Afisa Mtendaji wa kata ya Murufiti wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Cameroon Chugazo alisema hakuna kiongozi yeyote duniani ambaye anafikia ngazi ya juu kimamlaka bila kusimamia mabega ya mwanamke kwa sababu mwanamke ndiye anayeandaa kiongozi wa kesho.

“Hakuna mwanaume anafanikiwa kuwa juu kiuongozi bila kusimamia mabega ya mwanamke. Mwanaume hawezi kuwa bora bila mwanamke huyo anayetengeneza kiongozi wa kesho, haiwezekani mwanamke huyo huyo atengeneze kiongozi bora halafu yeye awe wa hovyo ‘Haiwezekani Orijino izae feki’,sasa kama wao wanatengeneza viongozi kwanini wao wasiwe viongozi?”,alihoji Chugazo.

“Mwanamke ana nguvu kuliko mwanamke. Mama ndiyo anatengeneza kiongozi ‘Hawezi kutengeneza kitu orijina akawa feki’ .Kutokana na kutambua nafasi ya mwanamke,ndiyo maana TGNP na wadau tumekuja na mpango wa kuwaambia wanawake kuwa wanazo sifa za kuwa viongozi katika jamii”,alisema.

Alisema kinachotakiwa sasa ni wanawake kuamka kifikra na kuachana na kauli za mawazo mgando kuwa mwanamke hawezi kuongoza bali wajitokeze kugombea na kushika nafasi za uongozi nchini.

Naye Mwenyekiti wa VIKOBA kata ya Kizengi wilaya ya Uyui mkoa wa Tabora, Hobokela Joseph aliwataka wanawake kupuuza kauli zinazowakatisha tamaa wanawake kugombea nafasi za ,uongozi kama vile kauli za kwamba ‘Mwanamke hawezi kuwa juu ya mwanaume’, ‘mwanamke akiwa kiongozi atachukua waume za watu’ ‘mwanamke akiwa kiongozi atakuwa mhuni na malaya’,’mwanamke ni wa kuzaa tu na kulea familia’.

Aidha aliwashauri wanawake kujiunga katika vikundi vya ujasiriamali/VIKOBA ili waweze kujikwamua kiuchumi ili kukabiliana na changamoto ya uchumi huku akiwataka wanawake kutoa sauti ili wasaidiwe pale wanapobaini wanakandamizwa katika jamii.

Kwa upande wake, Kiongozi wa Jamii Avelina Mwigulu kutoka wilaya ya Meatu mkoani Simiyu alisema bado kuna baadhi ya wanaume hawataki kuwaruhusu wanawake kugombea nafasi za uongozi kwa hofu ya kwamba mwanamke akiwa kiongozi atakuwa na mamlaka na nguvu zaidi kuliko mwanamke kitendo ambacho amesema siyo kweli.

“Nawaomba wanaume waachane na mtazamo huu hasi kwani masuala ya uongozi siyo nguvu bali kinachotakiwa ni akili,hekima na busara ambavyo hata wanawake wanavyo.Wanaume wawaunge mkono na kuwapa ushirikiano wanawake wawe katika nafasi za uongozi na ngazi za maamuzi ili tulete mabadiliko chanya katika jamii”,alisema Mwigulu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post