WADAU WA MICHEZO KILIMANJARO WAIPONGEZA TIGO KILI HALF MARATHON KWA KUIBUA VIPAJI VIPYA

Na TIGO TEAM, MOSHI.

WADAU mbalimbali wa michezo mkoani Kilimanjaro hususani wapenzi wa mchezo wa Riadha (Mbio) mkoani hapa wamepongeza mchango mkubwa unaofanywa na Mbio maarufu Afrika mashariki na duniani kwa ujumla za Tigo Kili Half Marathon katika kuibua vipaji mbalimbali vya Wanariadha wanaoiwakilisha vyema nchi ya Tanzania katika Medani mbalimbali za Mashindano ya Mbio kitaifa na kimataifa.

Wakizungumzia namna mbio hizo zimesaidia kuinua vipaji vya wanariadha waliofanya vyema katika Mashindano ya Mbio kitaifa na Kimataifa kama vile Emmanuel Giniki na Alphonce Simbu; wadau hao wanafafanua kuwa, Tigo Kili Half Marathon imewaibua wanariadaha wengi mmashuhuri na ina mchango mkubwa sana katika kukuza mchezo wa ridaha nchini.

Mbio za tigo Kili Half Marathon zimezinduliwa hivi karibuni mjini Moshi ambapo wadau mbalimbali kutoka katika mataifa mbalimbali duniani wanatarajiwa kumiminika mkoani Kilimanjaro zinatarajiwa kuleta neema kubwa ya kiuchumi mkoani hapa.

Mbio hizo zilizozinduliwa rasmi katika viwanja vya kibo Palace Homes, mjini Moshi kwa kuwashirikisha viongozi mbalimbali, wadhamini, Chama Cha riadaha mkoani Kilimanjaro (KAAA), waandaaaji wa mbio hizo na wadau mbalimbali zinatarajiwa kufanyika siku ya jumapili ya Machi 1, 2020 katika viwanja vya Chuo Kikuu Cha ushirika mjini Moshi (MoCU).

Akizungumzia namna mbio hizo zimesaidia kuinua vipaji vipya ikiwemo Wanariadha wapya waliofanya vizuri katika mashindano ya kitaifa na kimataifa, Mwenyekiti wa Chama Riadha Maniaspaa ya Moshi (MMAAA), Abdi Massawe anafafanua kuwa kwa kutambua mchango mkubwa unaofanywa na Tigo Kili Half Marathon, chama cahake kimepeleka wakimbiaji mahiri 17 kushiriki mashindano hayo ya kilometa 21 kwa mwaka huu wa 2020.

“Pia tutapeleka wakimbiaji mbalimbali zaia ya 60 kutoka katika makundi mbalimbali ikiwemo wakimbiaji binafsi na Jogging klabu mbalimbali zilizoko mkoani Kilimanjaro kushiriki mashindano ya Tigo Kili Half Marathon…” anafafanua Abdi Massawe.

Massawe amewataka wananchi mbalimbali mkonai hapa kujitokeza kwa wingi kushiriki mashindano ya Tigo Kili Half Marathon kwani mbali na kuibua vipaji mbalimbali vya wanariadaha wapya, pia yatawasaidia kuboresha afya zao kupitia michezo.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Aidan Komba alisema: “Tigo tunajivunia kuwa wadhamini wakuu wa mbio maarufu za Tigo Kili Half Marathon kwa mwaka wa nne mfululizo. Tukiongoza sokoni kwenye mageuzi ya maisha ya kidijiti yakiwamo masuala ya fedha, tunafurahi kwa mara nyingine tena kuwezesha usajili na malipo kwa washiriki kwenye mashindano hayo yajayo kupitia kwa huduma zetu kamilifu za fedha - Tigo Pesa.

Alisema kwamba kwa miaka kadhaa sasa, Tigo Pesa imethibitishwa kuwa bora zaidi na mfumo wa kuaminika wa malipo kwa wanariadha wote wenye nia kutoka sehemu yoyote nchini. “Zaidi ya hapo, tunakaribisha kila mmoja kwa ajili ya kupata kumbukumbu za mashindano hayo na kutumia wengine kupitia mtandao wenye kasi zaidi Tanzania wa 4G+,” akasema.

“Washiriki waendelee kujisajili kupitia mtandao na kufanya malipo kwa kutumia credit card kupitia https://ift.tt/1n0Lfq7 au kupitia TIGO Pesa - Pigal *149*20# kisha fuata maelekezo,” alisema na kuongeza kwamba washiriki wajisajili mapema ili kuepuka usumbufu kwani usajiliutafungwa Februari 16,2019 au nafasi zitakapojaa.

Mwisho.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527