ALIYETUMBULIWA KWA VYETI FEKI MIKONONI MWA POLISI KWA TUHUMA ZA KUUA MWANAFUNZI | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, February 12, 2020

ALIYETUMBULIWA KWA VYETI FEKI MIKONONI MWA POLISI KWA TUHUMA ZA KUUA MWANAFUNZI

  Malunde       Wednesday, February 12, 2020


Kamanda Revocatus Malimi

Jeshi la polisi mkoani Kagera linamshikilia Dezber Kahwa mwenye umri wa miaka 49 mkazi wa kijiji Kibengwe, Bukoba Vijijini kwa tuhuma za kusababisha kifo cha Alinda Leverian mwenye umri wa miaka 14.

Inaelezwa kuwa Mtuhumiwa huyo alimtoa mimba kwa njia isiyokuwa halali na salama mwanafunzi huyo wa darasa la sita Shule ya Msingi Kilima.

Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi amesema kuwa tukio hilo lilitokea Februari 08 mwaka huu nyumbani kwa Vedastina Cleophace, huku Kahwa ambaye alikuwa muuguzi katika zahanati ya Buza kabla ya kufukuzwa kazi na serikali wakati wa kuwaondoa watumishi hewa, kujaribu kumtoa mimba mwanafunzi huyo.

Mwili wa mwanafunzi huyo umefanyiwa uchunguzi na daktari wa binadamu katika hospitali ya Rufaa Bukoba na kubaini kuwa chanzo cha kifo hicho ni kutobolewa kwa mfuko wa uzazi na kuingizwa sumu.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post