MWANAJESHI KORTINI KWA KUMUUA MWANAJESHI MWENZAKE KWA RISASI 19


Askari wa JWTZ Wilayani Nachingwea, Lindi Pascal Lipita(28), amefikishwa Mahakamani akituhumiwa kumuua kwa kumpiga risasi Askari mwenzake ambaye ni Mpenzi wake Baserisa Ulaya.


Mtuhumiwa huyo alifikishwa jana mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa huo, Maria Batulaine, na kusomewa shtaka linalomkabili.


Mwanasheria wa Serikali, Abdulrahman Mohamed, alidai kuwa askari hao walikuwa na uhusiano wa kimapenzi na kwamba wivu ndio unaodaiwa kusababisha mauaji hayo.

Mwanasheria huyo wa serikali alidai kuwa mshtakiwa alifanya mauaji hayo Februari 10, mwaka huu, majira ya Saa 12;00 jioni wakiwa kambi ya Nang’ondo.

Alidai kuwa siku hiyo ya tukio, wakiwa kambini hapo, mshitakiwa akiwa na silaha, alimmiminia askari mwenzake risasi 19 kisha kuchakaza mwili wake na kumkatisha uhai.

Mshtakiwa amerejeshwa rumande na atarudi tena Makamani March 02, 2020 kesi itakapotajwa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post