RAIS WA ZAMANI WA MISRI HOSNI MUBARAK AFARIKI DUNIA | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, February 25, 2020

RAIS WA ZAMANI WA MISRI HOSNI MUBARAK AFARIKI DUNIA

  Malunde       Tuesday, February 25, 2020

Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak afariki dunia hospitalini jijini Cairo akiwa na miaka 91.

Mubarak alidumu madarakani kwa miongo mitatu kabla ya kung'atuliwa jeshi baada ya maandamano makubwa ya raia.

Alikutwa na hatia ya kula njama katika mauaji ya waandamanaji wakati wa mapinduzi na kuwekwa kizuizini.

Hata hivyo, hatia hiyo iliondolewa na akaachiwa huru mwezi Machi 2017.

Kifo chake kimethibitishwa na Televisheni ya taifa ya Misri leo Jumanne. Mapema tovuti ya Al-Watan iliripoti kuwa kiongozi huyo alifariki kwenye hospitali moja ya jeshi.

Mubarak alifanyiwa upasuaji mwishoni mwa mwezi Januari.

Mtoto wake wa kiume Alaa alisema siku ya Jumamosi kuwa baba yake yupo mahututi.

Je Mubarak alikuwa nani?

Baada ya kuzaliwa mwaka 1928, Mubarak aliingia jeshi kama kijana na kuendelea kuchukua jukumu muhimu katika vita kati ya Israel na Waarabu 1973.

Alikuwa rais chini ya muongo mmoja baadaye , kufuatia ,mauaji ya rais Anwar Sadat.

Alikuwa na jukumu muhimu katika mchakato wa amani wa Israel - Palestina.Hosni Mubarak katikati akiwa na viongozi wengine wa zamani akiwemo aliyekuwa rais wa Marekani Bill Clinton

Lakini licha ya mabilioni ya madola ya misaada ya kijeshi ambayo Misri ilipokea wakati alipokuwa madarakani , ukosefu wa ajira, ufukara, na ufisadi uliendelea kuimarika.

Mwaka mmoja baada ya Mubarak kupinduliwa , Mohammed Morsi mwanasiasa Muislamu , alishinda uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia nchini Misri.

Morsi yeye mwenyewe alitimuliwa madarakani na jeshi 2013 na kufariki 2019 akiwa jela.

Mubarak , wakati huohuo, alifungwa kifungo cha maisha kufuatia vifo vya waandamanaji 900 ambao waliuawa na vikosi vya usalama wakati wa maandamano ya 2011.

Mashtaka hayo baadaye yalifutiliwa mbali na Mubaraka kuachiliwa 2017

Mgogoro ulizuka mnamo mwezi Januari 2011, baada ya maandamano kama hayo kutokea Tuinisia na kusaidia kupinduliwa kwa rais wa taifa hilo.

Mubarak alilazimishwa kujiuzulu siku 18 baadaye.
Chanzo - BBC
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post