MBWA KOKO AZUA BALAA UWANJANI

Video moja imetrend sana mtandaoni ikimuonyesha mbwa koko akisitisha mechi baada ya kuingia uwanjani na kuchukua umiliki wa mpira wakati wa mechi jijini Istanbul.

Katika Video hiyo fupi ya mnamo Jumatano, Februari 18, mbwa huyo mweupe anaonekana akikimbia uwanjani wakati wachezaji walikuwa wanajiandaa kuanza mechi.

Kisha mbwa huyo aliuchukua mpira na kuanza kucheza nao na kuwaduwaza wachezaji, refa na hata mashabiki.

Juhudi za wachezaji kujaribu kuchukua mpira huo zilionekana kugonga mwamba.

Mchezaji mmoja alijaribu kupiga mpira huo nje ili kumfukuza mbwa huyo, lakini bado aliufuata na kurejea uwanjani.

Hatimaye mbwa huyo aliweza kuondolewa uwanjani na kupelekwa mahali salama na mmoja wa wachezaji kabla ya mechi hiyo kuendelea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post