LIPUMBA: HATUTASUSIA UCHAGUZI TENA....TUTAWEKA WAGOMBEA KOTE TANZANIA BARA NA VISIWANI | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, February 29, 2020

LIPUMBA: HATUTASUSIA UCHAGUZI TENA....TUTAWEKA WAGOMBEA KOTE TANZANIA BARA NA VISIWANI

  Malunde       Saturday, February 29, 2020

Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba, amesema kuwa pamoja na  Demokrasia Kuyumba  nchini lakini hawatasusia uchaguzi mkuu wa 2020, kama ilivyokuwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2019.

Prof Lipumba ameyasema hayo leo Februari 29, 2020, wakati wa kuhitimisha ziara yake katika mkoa wa Morogoro, ambapo amefanya Mkutano wa ndani katika Jimbo la Morogoro Mjini.

"Tutahakikisha tunakuwa na wagombea katika maeneo yote ya Tanzania bara na visiwani, kuanzia ngazi ya Urais, Ubunge, Udiwani na uwakilishi kwa upande wa Zanzibar', ameeleza.

Katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Novemba 24, 2019, CUF pamoja na vyama vingine vya siasa vilisusia uchaguzi huo.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post