ALGERIA YATHIBITISHA KUWA NA MGONJWA WA CORONA....WALIOFARIKI HADI SASA KWA VIRUSI HIVYO NI WATU 2,763


Algeria imethibitisha kisa cha kwanza cha virusi vya Corona, ambapo mgonjwa ni raia wa Italia aliyewasili nchini humo Februari 17. 


Tayari mgonjwa huyo amewekwa eneo maalumu la matibabu. 

Algeria inakuwa nchi ya pili ya Afrika kupata muathirika wa virusi hivyo baaada ya Misri.


Watu waliofariki  hadi sasa kwa virusi hivyo  Ulimwenguni wamefikia 2,763 huku Watu 80,970 wakiathirika
 

Wagonjwa 29,745 wamepona maambukizi hayo nchini China na kuruhusiwa kutoka hospitalini


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post