IGP SIRRO ATAKA WAZAZI WAIMARISHE MALEZI KWA WATOTO ILI KUWA NA JAMII INAYOCHUKIA UHALIFU


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Simon Sirro ametoa wito kwa jamii hasa wazazi nchini kuhakikisha wanaimarisha malezi ya watoto wao, jambo litalalosaidia kuwa na jamii itakayochukia uhalifu.

IGP Sirro ametoa wito huo mkoani Dodoma wakati akizungumza na baadhi ya Wakazi wa eneo la Mbande, baada ya kukagua ujenzi wa kituo cha polisi katika eneo hilo.

Amewashauri wazazi wote nchini kuendelea kuwasomesha watoto wao na kutowaacha wajiingize kwenye vitendo vya uhalifu.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527