WATU 17 WAFARIKI DUNIA NA 150 WAJERUHIWA KATIKA VURUGU MJINI NEW DELHI, INDIA


Watu 17 wamefariki dunia na wengine wapatao 150 wamejeruhiwa hapo jana katika makabiliano kati ya waandamanaji wa makundi yanayokinzana mjini New Delhi huko India. 


Makabiliano hayo ni mabaya zaidi kushuhudiwa tangu vurugu zilipozuka juu ya sheria mpya ya uraia mwanzoni mwa mwezi Desemba. 

Vurugu hizo zilianza tangu mwishoni mwa juma lakini ziligeuka kuwa mbaya zaidi Jumatatu iliyopita. 

Machafuko mapya yalianza tena jana Jumanne katika maeneo tofauti ya mji mkuu huo wa New Delhi. 

Afisa wa idara ya kukabiliana na majanga ya moto ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba timu yake imekuwa ikipokea simu za dharura za kwenda kuzima moto katika maeneo tofauti. 

Sheria hiyo mpya iliyozua ghasia inawapa fursa wahamiaji wasio Waislamu kutoka nchi tatu jirani kupata urai wa India.

 Waislamu nchini India wanadai kuwa ni sheria ya kibaguzi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527