VYOMBO VYA HABARI VYA MAREKANI VYADAI MAKOMBORA YA IRAN YALIITUNGUA NDEGE YA UKRAINE


Marekani wanaamini Ndege ya Abiria ya Ukraine 'Boeing 737 iliyoanguka Iran na kuua watu 176 ilitunguliwa kwa bahati mbaya na Iran.


Maofisa wa Marekani kwa mujibu wa runinga ya CBS wanasema mitambo ya Satellite imenasa makombora mawili ambayo yalirushwa kabla ya Ndege kuanguka yakifuatiwa na mlipuko mkubwa.


Ukraine awali ilisema kuwa inachunguza endapo ndege yake iliangushwa na kombora, jambo ambalo mamlaka za Iran zilikanusha vikali.

Kuanguka kwa ndege hiyo kulitokea saa chache baada ya Iran kushambulia kambi za kijeshi za Marekani nchini Iraq kwa makombora ya masafa marefu.

Rais wa Marekani Donald Trump siku ya Alhamisi alisema: "nina mashaka" juu ya (kuanguka) kwa ndege. "Inawezekana kuna mtu amefanya kosa kubwa."

Iran imetangaza kutokabidhi kisanduku cheusi cha kuhifadhi taarifa za ndege kwa kampuni ya ndege ya Boeing ama serikali ya Marekani kwa uchunguzi wa ajali hiyo.

Hatua hiyo inatokana na mzozo uliokomaa baina ya Marekani na Iran


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527