HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI YAJIVUNIA UBORA TIBA YA UPASUAJI NCHINI

Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji Hospitali ya Taifa Muhimbili-Upanga, Dkt. Sufian Baruani akizungumza na Maafisa Habari na Mahusiano wa Wizara ya Afya na taasisi zake na wanahabari (hawpao pichani) wakati wa mkutano huo.

Na Andrew Chale - Dar es salaam

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili imejivunia ubora unaotolewa katika Kurugenzi ya Upasuaji kwa kuongeza huduma nyingi pamoja na ubora wa mashine za kisasa ambapo wameokoa fedha nyingi kama Watanzania wangefuata huduma hiyo nje ya nchi.


Akizungumza katika ziara ya Maafisa  Mawasiliano kutoka Wizara ya Afya na Taasisi ya 'Tumeboresha Sekta ya Afya', Mkurugenzi wa huduma za upasuaji Dkt. Sufian Baruani alisema kwa kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya tano

Wameweza kufanya mambo mbalimbali ikiwemo upanuzi wa vyumba, ununuzi wa vifaa vipya zikiwemo mashine za kisasa sambamba na kuongeza wataalam wa kibingwa.

"Hospitali ya Taifa Muhimbili-Upanga tumefanya upanuzi wa vyumba vya upasuaji kutoka 11 hadi 20 na umepunguza wagonjwa kukaa muda mrefu kusubiria huduma hii.

Awali muda ulikuwa hadi wiki 6-8, kwa mfano idara ya watoto hivi sasa muda umepunhua hadi wiki 2" alisema Dkt. Baruani.

Katika kuongeza huduma, 2017 waliweza kuanzisha huduma ya kupandikiza vifaa vya usikivu na kuweza kuwafanyia Wagonjwa 34 na kugharimu shilingi Bilioni 1.2.

"Katika maboresho ya Sekta ya Afya. Muhimbili tulikuja na huduma hii ya kupandikiza vifaa vya Usikivu ambayo ni gharama sana kwa mgonjwa mmoja.

Kabla ya hapo tulikuwa tunapeleka wagonjwa nje ya nchi kwa gharama ya shilingi Milioni 100 kwa Mgonjwa mmoja ambapo kwa hapa Muhimbili sisi Mgo jwa mmoja anagharimu shilingi milioni.35." Alisema Dkt. Buriani.

Na kuongeza kuwa, toka mwaka 2003 hadi 2016 Serikali iliweza kupeleka wagonjwa 50 nchini India.

"Tumeweza kuokoa fedha nyingi sana. Wagonjwa 34 tuliowapa huduma hapa kwetu kama wangeenda nje gharama ingekuwa Bilioni 3.4, hivyo Hospitali imeokoa bilioni 2.2. 

Lakini pia awamu hii ya tano, Hospitali imenunua mashine ya kupima Usikivu (ABR) na kukarabato chumna cha usikivu" alisema Dkt. Buriani.


Katika kuhakikisha huduma zinakuwa bora zaidi kama hapa nchini, vifaa mbalimbali wameweza kuagiza ambapo vitakuwa msaada kwa Taifa katika uboreshaji wa huduma.

"Tumeagiza vifaa vyenye thamani ya milioni 800 kwa ajili ya upasuaji wa matundu madogo.

Pia tumeagiza vifaa vya shilingi milioni 700 ili kuboresha huduma za macho. Vifaa hivi ni kwa ajili ya kupima matatizo mbalimbali ya macho pamoja na vifaa vya kutengeneza miwani." Alisema Dkt. Baruani.

Dkt. Baruani ameongeza kuwa, katika huduma ya tezi dume, wameshanunua mashine ya kisasa yenye thamani ya milioni 70 , ambapo itasaidia kuchukulia vipimo vya tatizo hilo.

Kurugenzi hiyo ya upasuaji pia imeongeza viti viwili toka 7 hadi 9 pamoja na kununua vifaa vya maabara vya kutengenez meno ya bandia.

"Awali wagonjwa walikuwa wanaipata huduma hii ya meno bandia hospitali binafsi kwa sasa tumeimarisha.

Lakini pia kuna huduma hazikuwepo awali. Hizi ni huduma za matibabu za uvimbe wa taya (Haemangioma) kwa kutumia mionzi yaani interventional radiology ambapo toka mwaka 2017 hadi sasa wagonjwa 302 wamehudumiwa kwa gharama nafuu ya milioni 8 kwa kila Mgonjwa na endapo wangeenda nje ya nchi wangegharimu milioni 100 kwa mgonjwa mmoja.

"Huduma ya pili ni ya urekebishaji wa mifupa ya uso na taya ambapo hadi sasa wagonjwa 120 wamenufaika kwa grama ya shilingi milioni 3.5 kwa mgonjwa mmoja na endepo wangeenda nje ya nchi kwa kila mgonjwa mmoja angegharimu milioni 70." Alisema Dkt. Buriani.

Hata hivyo alieleza kuwa, Serikali ya awamu ya tano imeweza kusikia vilio vya wanyonge ambapo huduma zote zinazotolewa ni za kibingwa hivyo Watanzania waendelee kuwa na imani na Serikali yao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post