UINGEREZA YATOA TAHADHARI KWA RAIA WAKE KUTOSAFIRI IRAQ NA IRAN | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, January 4, 2020

UINGEREZA YATOA TAHADHARI KWA RAIA WAKE KUTOSAFIRI IRAQ NA IRAN

  Malunde       Saturday, January 4, 2020

Serikali ya uingereza hii leo imetoa onyo kwa raia wake kutosafiri kuelekea Iraq au kufanya safari za aina yoyote kuelekea Iran kufuatia kuuwawa kwa Qassem Soleimani, Kamanda wa kijeshi wa ngazi ya juu wa Iran. 

Ofisi ya Wizara ya mambo ya kigeni imesema kufuatia mvutano wa kikanda unaozidi kupamba moto, hivi sasa imewashauri raia wake kutosafiri kuelekea katika maeneo hayo isipokuwa tu eneo la Kurdistan.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza Dominic Raab amesema ni vizuri raia wa taifa hilo kufikiria kwa makini iwapo ni salama kwao kusafiri kuelekea Iran kwa sasa.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post