UBALOZI WA MAREKANI NCHINI IRAQ WASHAMBULIWA TENA


Marekani imeitolea mwito Iraq kulinda majengo yake ya kidiplomasia baada ya ubalozi wake mjini Baghdad kushambuliwa kwa maroketi matatu. 

Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani ametoa mwito kwenye taarifa yake kwa Iraq kutimiza wajibu wake wa kuyalinda majengo hayo. 

Jana Jumapili roketi moja lilishambulia eneo la kulia chakula kwenye ubalozi wa Marekani nyakati za chakula cha jioni, wakati maroketi mengine mawili yakiangukia karibu na eneo hilo, hii ikiwa ni kulingana na chanzo kilichozungumza na shirika la habari la AFP. 

Amesema tangu Septemba mwaka jana kumekuwepo na mashambulizi 14 yanayofanywa na wanamgambo wa Iran na wanaoungwa mkono na Iran dhidi ya watumishi wa Marekani waliopo Iraq. 

Amesema, hali ya usalama ni ya wasiwasi na makundi yenye silaha yanayoungwa mkono na Iran yanaendelea kusalia kitisho.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527