Masauni: ”Utaratibu wa kuzuia mikutano ya kisiasa isiyofuata sheria uko palepale”

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema, utaratibu wa kuzuia Mikutano ya Kisiasa isiyofuata Sheria na taratibu upo palepale

Amesema hayo akiwa Visiwani Zanzibar alipokuwa akizungumzia hali ya Usalama kwa kipindi cha Januari hadi Desemba 2019 visiwani humo

Amesema, muda wa Siasa ukifika Serikali itaruhusu mikutano hiyo yenye lengo la kutoa nafasi kwa Wanasiasa kuzungumza na Wananchi na kueleza kwa Wananchi walichokifanya kwa muda waliopewa baada ya kuchaguliwa na kuteuliwa katika nafasi mbalimbali

Kuhusu hali ya usalama kwa kipindi cha 2019, amesema matukio ya mauaji yamepungua kutoka 40 mwaka 2018 hadi 35 mwaka 2019 huku matukio ya udhalilishaji yakiongezeka kutoka matukio 15 mwaka 2018 mpaka matukio 35 mwaka 2019.


Amesema Serikali kupitia jeshi la polisi na mamlaka nyingine zinazohusika limeanza harakati za kudhibiti matukio  hayo  yanayosababishwa  na  mambo mbalimbali ikiwemo imani za kishirikina.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post