TANZANIA YAJIUNGA NA CHINA KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA MWAKA MPYA



Baadhi ya Watanzania wamejiunga na marafiki zao wa China kusherehekea sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa Kichina inayokaribia kwenye tamasha kubwa la Heri ya Mwaka Mpya wa Kichina 2020.


Shughuli hizo zimefanyika nchini Tanzania kwa miaka kumi mfululizo, ambazo zinaonesha kukaribia kwa mwaka mpya wa jadi wa kichina.

Kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Tanzania Mheshimiwa Samia Hassan Suluhu, Waziri wa nchi wa Tanzania Mheshmiwa  George Simbachawene amesema, watanzania wanafurahia kujumuika na wachina kusherehekea mwaka mpya wa jadi, pia amesema Tanzania na China ni marafiki wakubwa.

Habari pia zinasema mamia ya watu wa China na Afrika Kusini kutoka sekta mbalimbali jana walikusanyika kwenye Uwanja wa Nelson Mandela huko Johannesburg na kusherehekea mwaka mpya wa jadi wa kichina.

Wasanii wa China na Afrika Kusini walifanya maonesho ya Kung Fu, sarakasi, opera ya Sichuan na sanaa ya chai ya Kichina, na kuwavutia watazamaji.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527