TANZANIA NA UJERUMANI KUENDELEA KUSHIRIKIANA KATIKA SEKTA YA AFYA


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwa kwenye mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mhe. Regine Hess kwenye ofisi za wizara jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mhe. Regine Hess kwenye ofisi za wizara jijini Dodoma.

Katika Mazungumzo yao Waziri Ummy Mwalimu aliishukuru nchi hiyo kwa mashirikiano yao katika sekta ya afya hususan afya ya msingi kupitia shirika la GIZ na KFW toka mwaka 2003.

Naye Balozi Mhe.Regine amesema nchi yao itaendelea kuisaidia Tanzania katika kuwajengea uwezo watumishi wa afya na katika maeneo mengine katika nyanja za afya.

Tanzania na Ujerumani zimeanza mashirikiano toka mwaka 1961

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post