TAKUKURU MANYARA YAOKOA SHILINGI MILIONI 13


Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Manyara Fidelis Kalungura akitoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha kuanzia Oktoba 2019 hadi Disemba 2019 kwa waandishi wa habari

Beatrice Mosses - Malunde1 blog Manyara
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Manyara limefanikiwa imeokoa kiasi cha zaidi ya mil.13 kutoka idara mbalimbali kutokana  na uchunguzi uliofanywa na kubaini baadhi ya fedha zilitumika katika matumizi yasiyokuwa rasmi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Manyara Fidelis Kalungura alisema katika kipindi cha mwezi Oktoba hadi Desemba 2019  alisema licha ya kuokoa kiasi hicho la pia kwa kipindi hicho cha mwezi octoba hadi Desemba 2019 Takukuru ilipokea jumla ya malalamiko 175 huku TAMISEMI ikiongoza kwa kuwa na malalamiko 104.

Alisema Takukuru Manyara imejipanga kuzuia vitendo vya rushwa kwa kufuatilia fedha zinazotolewa na serikali pamoja na taasisi zisizokuwa za serikali kwa ajili ya miradi ya maendeleo na huduma za jamii kuanzia Bajeti hadi hatua ya utekelezaji.

"Jukumu hilo la ufuatiliaji wa fedha za umma katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo litahusisha wadau wote wa miradi husika ili kuhakikisha kuwa miradi inayotekelezwa inakidhi malengo yaliyokusudiwa",alieleza..

Aidha katika hatua nyingine Kalungura amesema kuwa kumekuwa na vitendo vya kikatili vya rushwa ya ngono hasa mashuleni na katika vyuo mbalimbali lakini wahanga wa majanga haya wanashindwa kutoa ushirikiano hivyo wao kama taasisi kuwa na kigugumizi katika kufuatilia jambo hili. 

Aliyataja maeneo mengine ambayo taasisi hiyo  itashughulikia kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo kwani rushwa ndani ya vyama vya siasa kuelekea uchaguzi mkuu,  rushwa kwenye miradi ya maendeleo na rushwa ndani ya vyama vya ushirika. 

"Rushwa ya ngono imeonekana kukithiri sana hususani maeneo ya kazi,  rushwa ya ngono imekuwa ikikithiri sana vyuoni na mashuleni na inapokuwa rushwa ya ngono imekithiri sana katika maeneo hayo matokeo yake tutapata wana taaluma wasiokuwa na taaluma sahihi, tutapata viongozi wasiokuwa na sifa,  tutapata watendaji wasiokuwa na sifa lakini mwisho wa siku rushwa hiyo hiyo inadhoofisha utendaji katika kazi",aliongeza. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post