MWANAMKE TAJIRI ZAIDI AFRIKA ATANGAZA KUGOMBEA URAIS

Isabel dos Santos ni mmojawapo ya wanawake matajiri zaidi duniani

Bilionea wa Angola Isabel Dos santos ambaye amegubikwa na kashfa kubwa ya fedha amesema kwamba huenda akawania urais wa taifa hilo.

Katika mahojiano na BBC Bi Dos Santos alipinga mara nne ya uwezekano wa yeye kutowania urais wa taifa hilo. Babake Jose Eduardo dos Santos aliiongoza Angola kwa miaka 38.

Waendesha mashtaka wako katika harakati ya kukomboa $1bn (£760m) ambazo bi Dos Santos na washirika wake wanadaiwa na serikali.

Bi dos Santos , mwenye umri wa miaka 46 ni mmojawapo wa wanawake matajiri zaidi duniani, huku jarida la Forbes likikadiria mali yake kuwa yenye thamani ya $2.2bn, hatua inayomfanya kuwa mwanamke tajiri zaidi barani Afrika..

Babake alimchagua kwa utata kuongoza kampuni ya mafuta nchini Angola inayomilikiwa na serikali ya Sonangol mwaka 2016.

Alifutwa kazi mwaka 2017 na rais Joao Lourenco , mrithi aliyechaguliwa na babake.
Alisema nini?

Katika mahojiano mjini London , aliripotiwa akisema kwamba maisha yake yapo hatarini iwapo atarudi nchini Angola katika hali ilivyo.

''Kuongoza ni kuhudumu, hivyobasi nitafanya ninachoweza maishani mwangu'' , alisema.

Bi Dos Santos baadaye aliambia runinga ya Ureno kwamba kuna uwezekano atawania urais 2022.

Tangazo hilo liliadhimisha mabadiliko kwa mwanamke ambaye amejitaja kuwa mfanyabiashara asiye na hamu ya kufanya siasa.José Eduardo dos Santos (kushoto) alimpatia madaraka Joao Lourenço 2017

Mahakama moja katika mji mkuu wa Angola Luanda mwezi uliopita iliagiza kupigwa tanji kwa akaunti yake ya benki na biashara yake katika taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta, kufuatia misururu ya uchunguzi kuhusu madai ya ufisadi uliofanywa dhidi ya na familia ya dos Santos ambayo waendesha mashtaka wanasema imelipokonya taifa hilo zaidi ya dola bilioni mbili.

''Haya ni madai ya uongo na huu ni mpango wa kisiasa wa serikali iliopo'', alisema.

Nduguye wa kambo Jose Filomeno Dos santos anakabiliwa na kesi nchini Angola kutokana na mashtaka ya ufisadi.

Upande wa mashtaka unadai kwamba yeye na wenzake walisaidia kupeleka nje ya nchi $500m wakati alipokuwa mkuu wa hazina ya Angola .

Wamekana kufanya makosa

Je Isabel dos Santos ni nani?
Mwana mkuu wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Jose Eduardo Dos Santos
Ni mke wa mfanyabiashara wa Congo Sindika Dokolo
Alihudumu katika shule ya upili ya wasichana ya mabweni nchini England.

Alisomea uhandisi wa umeme katika chuo kikuu cha Kings College mjini London.

Akiwa na miaka 24 alikuwa akimiliki hisa katika mgahawa wa Miami Beach uliopo mjini Luanda
Aliinuka na kuwa mwanamke tajiri zaidi barani Afrika
Alichaguliwa kuongoza shirika kuu la mafuta nchini Angola la Sonangol 2016 na kufutwa kazi 2017.

Ana hisa za asilimia sita katika mafuta ya Ureo na kampuni ya gesi ya galp ambayo ni thamani ya $830m
Anamiliki 42.5% ya benki ya Portugal ya Eurobic bank
Ana asilimia 25% ya hisa katika kampuni ya simu ya Unitelnchini Angola
Pia ana 42.5% ya hisa katika benki ya Angola kwa jina Banco BIC

Duru jarida la: Forbes namwengine

Ni nini kilichobadilika Angola?

Bi Dos Santos alimshutumu mara kwa mara rais Lourenco ambaye alimrithi babake miaka miwili iliopita kama rais.

Licha ya kutoka katika chama kimoja , cha MPLA amewashangaza raia wengi wa Angola kwa kuonekana akiilenga familia ya Dos Santos ikiwa mojawapo ya mikakati yake ya kupambana na ufisadi.

Bwana Lourenco anapigania kuwa na madaraka. Kuna mpango wa kupunguza uwezo au ushawishi uliokuwa na aliyekuwa rais wa taifa hilo katika chama cha MPLA , alisema Bi Dos Santos.

''Iwapo kutakuwa na mgombea tofauti kabla ya uchaguzi mkuu wa 2021 ambaye ataungwa mkono na rais wa zamani Jose dos Santos ama washirika wanaohusishwa naye hiyo itatoa changamoto kuu kwa bwana Lourenco kwa kuwa rekodi yake ni mbaya sana , aliongezea, akidai ukosefu wa ajira , uchumi uliozorota na msururu wa migomo''.

Lakini madai ya ufisadi yanayomlenga bi dos Santos na nduguye wa kambo yamepewa uzito mpya na tume ya kukabiliana na uhalifu ambayo ilizinduliwa dhidi yake nchini Angola.

''Ukweli ni kwamba kuna ushahidi mwingi dhidi yake . Ni mtu muhimu katika familia ya Dos Santos na tisho kubwa kwa Lourenco'' , alisema Daria Jonker mchanganuzi wa kieneo wa kundi la Eurasia , ambaye amesema kwamba madai ya ufisadi yalikuwa yakitumiwa na serikali kama mojawapo ya vita ndani ya chama cha MPLA.

''Lourenco anatuma ujumbe kwamba kuna kiongozi mpya akiwa na sheria mpya'', alisema bwana Jonker.José Filomeno dos Santos anakabiliwa na kesi ya ufisadi

Bi Santos alisisitiza kuwa anatumika kama 'kafara' na rais Lourenco na kushutumu idara ya mahakama ya Angola , akimlaumu mwanasheria mkuu kwa kudanganya na kukataa mawakili wake kuona ushahidi uliopo.

''Najuta kwamba Angola imetumia njia hii . Nadhani sote tutapoteza mengi, kiobngozi mzuri ni kiongozi mzuri'' , alisema akitaka kufanyika kwa mazungumzo ili kupata suluhu ya kisiasa kuhusu hali inayomkabili mbali na uharibifu zaidi wa uchumi wa Angola.
Je anaweza kushinda uchaguzi?

Lakini je yeye ama mshirika wake anaweza kumuondoa rais aliyepo madarakani?

''Mimi ni mfanyabiashara . watu wengi wananipenda na kunielewa ninachofanya na kuamini ninachodfanya. Kuna watu wengi ambao tuliwapatia kazi zao za kwanza '', akisifu biashara zake na kukana madai kwamba utajiri wake ulitokana na mali ya babake .Uchumi wa Angola umeimarika kwa sababu ya mafuta

Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post