SINGIDA UNITED NOMAAA!! YASAJILI KIKOSI KIZIMA..WOTE WAPYAAAA | MALUNDE 1 BLOG

Friday, January 17, 2020

SINGIDA UNITED NOMAAA!! YASAJILI KIKOSI KIZIMA..WOTE WAPYAAAA

  Malunde       Friday, January 17, 2020

Baadhi ya wachezaji wa Singida United

Ikiwa ziimepita siku mbili tangu dirisha dogo la usajili Tanzania kufungwa, tumeshuhudia klabu kadhaa zikifanya mabadiliko ya vikosi yao kwa kuongeza baadhi ya wachezaji na kuwaleta wengine wa kuziba nafasi hizo.

Klabu kubwa za Tanzania, Azam FC, Yanga na Simba zimefanya mabadiliko kadhaa ya vikosi vyao, ambapo Yanga imesajili wachezaji sita wapya, Simba ikisajili wachezaji wawili na Azam FC ikisajili wachezaji wawili.

Klabu ya Singida United imetia fora kwenye dirisha hili la usajili, ikiwa imesajili jumla ya wachezaji 11 ili kuongeza nguvu kwenye kikosi chao baada ya kugundua kuwa katika mzunguko wa kwanza kikosi chao kilikuwa dhaifu kwani kilikuwa na vijana wengi.

Wachezaji waliosajiliwa na Singida United ni George Sangija, Raphael Daud, Haruna Moshi Boban, Tumba Swedi, Haji Mwinyi, Owen Chaima, Ame Ally, Six Mwasekaga, Athumani Idd Chuji na Cleofas Sospeter.

Singida United iko katika nafasi ya 19 ya msimamo wa ligi kwa pointi 11, ikiwa imeshuka dimbani mechi 16 na kushinda mechi mbili pekee, ikifungwa mechi tisa na droo tano. Ikumbukwe kuwa msimu huu zitashuka jumla ya timu sita za ligi kuu huku zikipanda timu mbili pekee, kwakuwa msimu ujao ligi kuu Tanzania Bara itahusisha timu 16.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post