BABA AMPA UJAUZITO BINTI YAKE WA DARASA LA NNE...ATOWEKA NAYE KUSIKOJULIKANA


Mkazi wa kijiji cha Milala Kata ya Misunkumilo Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi aitwaye Deus Richard (40) anadaiwa kumpa ujauzito binti yake wa Darasa la Nne (jina linahifadhiwa) na kumtelekeza mkewe na watoto wadogo watano na kutoweka kusikojulika na mtoto wake aliyempa mimba.

Bi Mariam Masanja ambaye ndiye Mke aliyetelekezwa, amesema kuwa alipobaini uhusiano wa kimapenzi baina ya mwanae na Baba yake aliwaeleza viongozi wa Dini, kitendo ambacho kilimkasirisha bwana huyo na kuanza kuonesha bayana mapenzi yake na mtoto wake.

Aidha Mariam ameongeza kuwa licha ya ugumu wa maisha anaopitia kwa sasa, kutokana na kutelekezwa akiwa na watoto wadogo na pia ndani kukiwa hakuna chakula, anaiomba Serikali kumkamata mumewe na kumchukulia hatua kali za kisheria.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527