Simbachawene Agoma Kufungua Machinjio Ya Msalato jijini Dodoma | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, January 22, 2020

Simbachawene Agoma Kufungua Machinjio Ya Msalato jijini Dodoma

  Malunde       Wednesday, January 22, 2020
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene hii leo amegoma kufungua machinjio ya Msalato jijini Dodoma kwa kutokidhi vigezo vya ubora vinavyoridhisha ikiwemo ukarabati wa kiwango cha chini na kutoa muda wa wiki ya moja kurekebisha dosari zilizobainika.
 
Ametoa uamuzi huo wakati akitembelea jengo la machinjio ya Msalato jijini Dodoma wakati wa ziara aliyoifanya na kubaini kasoro mbalimbali zinazotakiwa kupatiwa ufumbuzi. “Sifungui hii machinjio kwa sababu hamjajiandaa na ujenzi uko hovyo kwahiyo siwezi kufungua kitu cha hovyo namna hii” Simbachawene alisisitiza.
 
Akiongea katika ziara hiyo amesema amesikitishwa sana na ukarabati wa kurekebisha machinjio hayo kwani haukidhi viwango na ujenzi wake ni wa kiwango cha chini hivyo amemuagiza Afisa Mipango Miji wa Jiji la Dodoma Bwana Shabani Juma kuhakikisha ndani ya wiki ya moja kila kitu alichotolea maelekezo kifanyiwe marekebisho.
 
“Sijafurahishwa kwa kwakweli, majengo ya Serikali yanatakiwa kujengwa na mafundi classic, vitu vya Serikali viwe State of Art” Simbachawene alisisitiza.
 
Waziri Simbachene pia amegiza kuandaliwa kwa taarifa rasmi ya ukarabati huo ikiwa ni pamoja na thamani ya fedha zilizotumika katika zoezi zima la ukarabati na ujenzi wa  mifumo ya maji safi na maji taka.
 
Naye Diwani wa Kata ya Msalato Mheshimwa. Ali Mohamed amesema kuwa amesikitishwa sana kwa kutofunguliwa kwa machinjio hiyo kwani wakazi wengi wa Kata yake wanategemea machinjio kwa shughuli zao za kila siku kwa sababu ni Wafugaji. Pia alisema Maelekezo yote yaliyotolewa na Mheshiwa Waziri Simbachawene wameyapokea na naamini kuwa yatarekebishwa kwa wakati.
 
Machinjio hiyo ya Msalato ilifungwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimazi wa Mazingira (NEMC) tarehe 31 Oktoba 2019 kutokana na sababu za mazingira yasiyokua safi na salama, kufuatia ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post