SERIKALI YAONYA WANANCHI WANAOJENGA MIJINI BILA KUFUATA UTARATIBU


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ameonya wananchi wanaojenga mijini bila kufuata utaratibu.

Mhe. Lukuvi ametoa kauli hiyo Jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na Wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mtaa wa Ndachi Kata ya Mnadani jijini Dodoma wakati akikagua nyumba ambazo zimejengwa bila kufata utaratibu na kukosa vibali vya ujenzi.

Waziri Lukuvi alifikia hatua ya kusimamisha ujenzi kwa kuziwekea alama nyumba ambazo ujenzi wake umekiukwa na kuwaamuru wamiliki kusitisha shughuri zote hadi wafuate utaratibu.

Hata hivyo Mhe. Lukuvi amesema Serikali haina mpango wa kubomoa nyumba za wananchi isipokuwa wananchi wanatakiwa kujenga kwa kufuata utaratibu ikiwa ni pamoja na kupata kibali cha ujenzi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post