RAIS WA IRAN HASSAN ROUHANI AIONYA MAREKANI KUHUSU KULIPA KISASI


Rais wa Iran Hassan Rouhani ameionya Marekani kufikiria mara mbili kabla haijalipiza kisasi cha shambulizi la Iran kwenye kambi ya Marekani iliyopo Iraq ambalo pia lilikuwa la kisasi dhidi ya mauaji ya jenerali wa vikosi maalumu vya Iran Qassemi Soleimani. 


Rouhani amenukuliwa akisema iwapo Marekani inapanga mashambulizi zaidi na uhalifu dhidi ya Iran watalipiza kisasi na mashambulizi makubwa zaidi, huku akilishukuru jeshi la walinzi wa amani kwa jibu hilo la kishujaa kwa Marekani. 

Ameliita shambulizi dhidi ya Soleimani kuwa ni uhalifu wa kivita wa Marekani ambao umewaleta pamoja zaidi watu wa Iran.

Spika wa bunge la Iraq Mohammed al-Halbusi amelaani mashambulizi hayo ya Iran aliyoyataja ni ukiukwaji wa uhuru wa taifa hilo. 

Ametoa mwito wa hatua za dharura za kuiepusha Iraq kuwa uwanja wa vita wa mataifa ya nje ikiwa ni pamoja na Iran.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527