KITUO KIKUBWA CHA HIJA CHATUA MKOANI SINGIDA

Askofu  wa Kanisa Katoliki Jimbo la Singida, Mhashamu Edward Mapunda  akizindua kituo cha Hija eneo la Sukamahela Singida.

Mamia ya wananchi wakipanda jiwe kuelekea katika kituo cha Hija  kwa ajili ya Hija maalum.
Mkuu wa Mkoa wa Singida  Dkt Rehema Nchimbi akitoa  salaam maalum za mkoa  wakati wa uzinduzi wa kituo cha hija Sukumahela
 Askofu  wa Kanisa Katoliki Jimbo la Singida, Mhashamu Edward Mapunda  akimnyunyizia maji ya Baraka Mkuu wa Mkoa wa Singida kwenye misa hiyo.

Na  John Mapepele
SINGIDA
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amesema uzinduzi  wa kituo kikubwa cha kihistoria cha Hija na Maombezi cha Bikira Maria kilijengwa  eneo la  Sukamahela ambalo ndiyo eneo la katikati ya nchi ya Tanzania kijiografia  wilayani Manyoni mkoani Singida  utabadilisha  uchumi na kuchochea maendeleo ya wananchi katika kipindi kifupi kijacho endapo wananchi watachangamkia fursa za uwekezaji katika eneo hili.

Dkt. Nchimbi ametoa rai hiyo leo kwenye mkutano na watumishi wa umma  ambapo amesema uzinduzi wa kituo hicho  unaifanya nchi  yetu kuongeza idadi ya vivutio vya utalii wa imani  ambavyo havikuwepo kabisa  hapa nchini hivyo kuvutia wageni kutoka ndani na nje ya nchi wanaokuja kutembelea vivutio mbalimbali kujumuisha eneo hilo.

Amewataka kwa wananchi  Mkoa wa Singida  na watanzania  kufanya uwekezaji katika eneo hilo kwenye sekta za utoaji wa huduma  ili kunufaika na wageni wanafika kujihi kutoka sehemu mbalimbali duniani na kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli za kuwaletea maendeleo watanzania.

 “Uzinduzi wa kituo cha Hija cha Bikira Maria siyo tu kwamba  utabadilisha kabisa uchumi wa watu wetu bali utasaidia nchi yetu kukuza amani ambayo ni mhimili mkuu wa maendeleo ya taifa lolote duniani” aliongeza dk. Nchimbi

Wakati huo huo Kanisa  Katoliki nchini  limetoa  pongezi na shukrani mahususi kwa Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi kwa kuwa na maono ya kiroho ya kubuni wazo la kuwa na kituo hicho na kuliwasilisha  kwa  kanisa  katoliki hatimaye kujengwa na kuzinduliwa kituo hicho katikati ya nchi ya Tanzania.
Akizindua kituo hicho Januari Mosi, Mwaka huu katika ibada maalum iliyofanyika eneo la Sukamahela,  Askofu  wa Kanisa Katoliki Jimbo la Singida, Mhashamu Edward Mapunda  kwa  niaba ya Kanisa Katoliki  nchini  alishukuru na kupongeza wazo la Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi ambapo pia alihimiza watanzania kutumia mwaka huu kwa sala na maombi wakati Taifa likielekea kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani, huku akiwasihi Wakristo nchini kote kumtumia Mama Bikira Maria ili aweke uchaguzi huo kwenye Moyo wake mtakatifu kwa sababu yeye ni Malkia wa Amani.
Maria alikuwa mwanamke Myahudi aliyeishi kati ya karne ya 1 KK na karne ya 1 BK. Mke wa Yosefu, alimzaa Yesu Kristo. Kwa sababu hiyo na kwa utakatifu wake anapewa heshima ya pekee katika madhehebu mengi ya Ukristo, lakini pia katika Uislamu duniani kote.
Wakiongea kwa nyakati tofauti  siku ya uzinduzi wa kituo hicho wananchi wa Sukamahela   walisifu na kupongeza ubunifu wa Mkuu wa Mkoa  katika mambo mbalimbali katika taifa letu.

“Ndugu yangu  kwa kusema  ukweli  tunamshukuru sana  mungu kwa  kumpa Mkuu wetu wa Mkoa  wa Singida mama Nchimbi maono yanayoleta mapinduzi ya kiroho, kiuchumi na kijamii maana  amefanya mapinduzi makubwa  pia katika kilimo cha Korosho”alilisitiza  Eliakimu  Joseph ambaye ni mkazi wa Manyoni
Naye Jummanne Mwenda  mkazi wa Singida mjini amesema kuwa mageuzi kama ya korosho aliyafanya Dkt. Nchimbi akiwa mkoani Njombe ambapo  alihamasisha  kilimo cha parachichi ambacho wananchi wa  mkoa huo wameendelea kunufaika nacho hadi sasa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527