POLISI TABORA KUANZA MSAKO WA WANAOTAKA KUJINYONGA 2020...."TUTAWAKAMATA KABLA HAWAJAJINYONGA"


Baada ya kupokea taarifa ya Watu wawili kujinyonga mpaka kupoteza maisha Tabora, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Barnabas Mwakalukwa amesema Polisi wataanza msako wa kuwabaini na kuwakamata wote wanaotarajia kujinyonga mwaka huu na kuwapelekea Mahakamani.




Kwa mujibu wa RPC Mwakalukwa, walijionyonga ni  Mwalimu Basil Sungu (39) wa shule ya msingi Ikongolo Wilaya ya Uyui mkoani Tabora ambaye  amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kipande cha kitenge cha mke wake.

Amesema mwili wa Sungu ulikutwa chumbani kwake ukiwa unaning’inia darini Jumanne iliyopita ya Desemba 31, 2019.



Mwingine ni James Albert (22), mjasiriamali na mkazi wa kata ya Chemchem Manispaa ya Tabora ambaye amekutwa amejinyonga hadi kufa kwa kutumia mkanda wa begi.



“Niwambie mwaka huu tabia hizo zikome kwa wanaotegemea kujinyonga tutaanzisha doria kuhakikisha wote wanaotarajia kujinyonga mwaka huu tunawakamata kabla hawajinyonga na tunawapelekea mahakamani” Amesema RPC  Mwakalukwa huku akisema uchunguzi dhidi ya matukio haya mawili unaendelea ili kujua chanzo


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527