MTOTO ATUHUMIWA KUMUUA BABA YAKE LUDEWA

Na Amiri Kilagalila-Njombe

Mzee Jonaidi Haule (72) mkazi wa Mawengi wilayani Ludewa Mkoani Njombe amesababishiwa kifo kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali na mwanae kutokana na ugomvi wa kifamilia.

Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema baada ya ugomvi kuibuka na kusababisha  hali ya kuto kuelewana kati ya mtoto na baba yake, ,mtoto aliyefahamika kwa jina la Jailos Thomas Haule alichukua kitu chenye ncha kali na kumjeruhi baba yake.

Kamanda amesema mara baada ya kujeruhiwa mzee huyo alifikishwa  katika matibabu hospitali ya wilaya ya Ludewa na kupoteza maisha mara baada ya hali yake kuwa mbaya zaidi.

Aidha kamanda wa polisi amesema jeshi hilo linamtafuta mtuhumiwa Jailos Haule aliyetokomea kusikojulikana kwa tuhuma za kesi ya mauaji.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post