IRAN YAAPA KULIPIZA KISASI KWA MAREKANI KUFUATIA MAUAJI YA KAMANDA MKUU WA JESHI LAKE LA QUDS | MALUNDE 1 BLOG

Friday, January 3, 2020

IRAN YAAPA KULIPIZA KISASI KWA MAREKANI KUFUATIA MAUAJI YA KAMANDA MKUU WA JESHI LAKE LA QUDS

  Malunde       Friday, January 3, 2020

Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei amesema, nchi hiyo itajibu vikali mauaji ya kamanda wa Kikosi cha Mapinduzi ya Kiislam (IRGC) Meja Jenerali Qassem Soleimani.

Khamenei amesema lengo la Soleimani na harakazi zake za ukombozi hatitasimama kutokana na kifo chake, bali zitaendelea kwa nguvu zaidi, na ushindi dhahiri unawasubiri wale wanaopigana katika njia hiyo.

IRGC leo imethibitisha kuwa, Meja Jenerali Soleimani ameuawa katika shambulizi la anga lililotokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad.

Kiongozi huyo ametangaza siku tatu za maombolezo kufuatia kifo cha Soleimani.

Wakati huohuo, Wizara ya Ulinzi ya Marekani imesema, jeshi lake lilifanya shambulizi lililomuua kamanda huyo wa IRGC.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post