Picha : WAZIRI WA MAJI PROF. MBARAWA AZINDUA BODI MPYA YA SHUWASA...AAGIZA WAKUSANYE MIL 700 KILA MWEZI

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa amezindua rasmi Bodi Mpya ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga Mjini (SHUWASA) na kuagiza Mamlaka hiyo kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato akitishia kuvunja bodi hiyo endapo watashindwa kukusanya shilingi milioni 700 kila mwezi.



Prof. Mbarawa amezindua Bodi mpya ya SHUWASA leo Alhamis Januari 9,2020 katika ofisi za SHUWASA zilizopo Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa maji kutoka ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga.

Akizindua bodi hiyo ya nane tangu SHUWASA ianzishwe mwaka 1998, itayoongozwa na Bi. Mwamvua  Jilumbi, Prof. Mbarawa aliitaka SHUWASA kukusanya mapato na kupanua mtandao wa maji kwa kujenga miradi yenye ubora ili kuondoa changamoto ya maji kwa wananchi.

“Kazi ya kwanza ambayo natoa kwa bodi hii mpya ni kwamba nataka mkusanye mapato yasiyopungua shilingi milioni 700 kila mwezi,mkishindwa kukusanya sitakuwa na msalie mtume kuvunja bodi hii”,alisema Prof. Mbarawa.

“Pesa mtakayokusanya muitumie kulipa KASHWASA na kupanua mtandao wa maji siyo kila siku mje kuomba fedha Wizarani. Fedha mnayopata ipelekeni kwenye miradi na mjenge miradi hiyo nyinyi wenyewe kwa kutumia wakandarasi wa ndani”,aliongeza Prof. Mbarawa.

Waziri huyo wa Maji aliitahadharisha bodi mpya ya SHUWASA kutothubutu kutumia fedha za mapato kujilipa posho na kupeana safari zisizo na tija akisema SHUWASA siyo mahala pa kula fedha bali ni kwa ajili ya kusaidia wananchi wapate maji safi, salama na ya kutosha.

“Naagiza bodi hii iwe inafanya maamuzi kwa wakati,msukume maamuzi yenu yafanyike kwa haraka kwani Watanzania wamechoka wanataka maji”,aliongeza.

Katika hatua nyingine alisema changamoto ya Taasisi za serikali ikiwemo Jeshi la Wananchi (JWTZ), polisi na Magereza kudaiwa na SHUWASA wanaifanyia kazi na serikali itawalipa huku akishauri taasisi hizo kufungiwa mita za malipa ya kabla ‘ Prepaid Meter’.

Akitoa taarifa ya Mwenyekiti wa Bodi ya SHUWASA iliyomaliza muda wake ambayo ilizinduliwa Novemba 14,2016,Deogratius Sulla,alisema taasisi za serikali hasa idara ya ulinzi na usalama zinasuasua katika kulipa ankara zake za maji kila mwezi,jambo ambalo linasababisha deni la maji kukua na kufikia shilingi milioni 949 akieleza kuwa jitihada za kufuatilia madeni hayo hazijazaa matunda makubwa hivyo kumuomba Waziri awasaidie kutatua changamoto hiyo.

"Mpaka mwezi Desemba 2019, JWTZ ilikuwa inadaiwa shilingi 520,244,975.50/=, Magereza shilingi 256,520,120.50/= na polisi shilingi 172,346,465/=",alieleza .

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Flaviana Kifizi, alisema hivi sasa mamlaka imeongezewa maeneo mengine matatu ya kutoa huduma ambayo awali yalikuwa yanahudumiwa na RUWASA ambayo ni Tinde,Didia na Iselamagazi.

Alisema SHUWASA hukusanya mapato ya wastani wa shilingi 497,891,531 kwa mwezi ambacho asilimia tano tu hutumika katika kuongeza mtandao katika maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma ya maji safi.

Kifizi alieleza kuwa SHUWASA inahuhudumia wakazi wa Manispaa ya Shinyanga wapatao 186,671 ambapo hadi sasa jumla ya wakazi 149,710 sawa na asilimia 80.2 wamefikiwa na huduma ya maji safi.

“Hadi kufikia Desemba 2019 Mamlaka ilikuwa na wateja wapatao 21,505 na mtandao wa maji safi wenye jumla ya kilomita 549.12. Mahitaji ya maji safi kwa wakazi wa Manispaa ya Shinyanga yanakadiriwa kuwa mita za ujazo 21,266 kwa siku”,alieleza Kifizi.

“Wastani wa matumizi ya maji kwa siku ni mita za ujazo 12,500 kwa siku sawa na asilimia 58.8 tu ya maji kwa manispaa yote.Kwa mwezi Desemba 2019 mamlaka ilisambaza maji yenye mita za ujazo 324,357 sawa na wastani wa mita za ujazo 11,709 kwa siku”,alisema Kifizi.

Aliongeza kuwa SHUWASA inasimamia na kujenga miradi kwa kutumia wataalamu wa ndani 'Force account' katika wilaya za Shinyanga (Negezi – Mwawaza) na Kahama (Ngogwa – Kitwana) ambapo Miradi hiyo inahusisha ujenzi wa matenki na mtandao wa maji safi.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa (mwenye suti ya bluu) akiwasili katika ofisi za Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga Mjini (SHUWASA) kwa ajili ya uzinduzi wa Bodi Mpya ya SHUWASA leo Alhamis Januari 9,2020. Wa kwanza kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA, Bi. Flaviana Kifizi. Wa kwanza kulia mbele ni Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Bw. Albert Msovela. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa akizungumza wakati akizindua rasmi Bodi Mpya ya SHUWASA. Wa kwanza kulia ni Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akifuatiwa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Stephen Masele na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga,Gulam Hafeez Mukadam.
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa akizungumza wakati akizindua rasmi Bodi Mpya ya SHUWASA na kuitaka bodi hiyo kufanya kazi kwa uadilifu ili kuwaisaidia wananchi ambao wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya maji.
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa akizungumza wakati akizindua rasmi Bodi Mpya ya SHUWASA.
Wakurugenzi wa Mamlaka mbalimbali za Maji nchini wakimsikiliza Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa.
Wakuu wa taasisi mbalimbali na wafanyakazi wa SHUWASA wakimsikiliza Waziri wa Maji Makame Mbarawa.
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack wakati uzinduzi wa bodi mpya ya SHUWASA.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Flaviana Kifizi akitoa taarifa kuhusu kazi  zinazofanywa na SHUWASA.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Flaviana Kifizi akitoa taarifa kuhusu kazi  zinazofanywa na SHUWASA.
Wafanyakazi wa SHUWASA wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea.
Mwenyekiti wa Bodi ya SHUWASA iliyomaliza muda wake Deogratius Sulla, akitoa taarifa kuhusu bodi iliyomaliza muda wake.
Mwakilishi wa wafanyakazi wa SHUWASA,Paulina Shagile akitoa taarifa ya wafanyakazi wa  SHUWASA.
Wadau wa maji wakiwa eneo la tukio.
Wafanyakazi wa SHUWASA wakiwa kwenye uzinduzi wa bodi mpya ya SHUWASA.
Wadau wa maji wakiwa kwenye uzinduzi wa bodi mpya ya SHUWASA.
Wadau wa maji wakiwa kwenye uzinduzi wa bodi mpya ya SHUWASA.
Wafanyakazi wa SHUWASA wakiwa kwenye uzinduzi wa bodi mpya ya SHUWASA.
Wafanyakazi wa SHUWASA wakiwa kwenye uzinduzi wa bodi mpya ya SHUWASA.
Wadau wa maji wakiwa kwenye uzinduzi wa bodi mpya ya SHUWASA.
Wafanyakazi wa SHUWASA wakiwa kwenye uzinduzi wa bodi mpya ya SHUWASA.
Wadau wa maji kutoka taasisi mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi wa bodi mpya ya SHUWASA.
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa akikabidhi zawadi kwa Mwenyekiti wa Bodi ya SHUWASA iliyomaliza muda wake, Deogratius Sulla wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga Mjini (SHUWASA). 
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa akikabidhi zawadi kwa Aliyekuwa Katibu wa Bodi ya SHUWASA iliyomaliza muda wake, Eng'. Silvester Mahole wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga Mjini (SHUWASA). 
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa akikabidhi vitendea kazi kwa Mwenyekiti wa Bodi ya SHUWASA Bi. Mwamvua Jilumbi wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga Mjini (SHUWASA). 
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa akikabidhi vitendea kazi kwa Mjumbe wa  Bodi ya SHUWASA,Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga Mjini (SHUWASA). 
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa akikabidhi vitendea kazi kwa Mjumbe wa  Bodi ya SHUWASA,Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Geofrey Mwangulumbi wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga Mjini (SHUWASA). 
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa akikabidhi vitendea kazi kwa Mjumbe wa  Bodi ya SHUWASA,Ziporah Pangani wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga Mjini (SHUWASA). 
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa akikabidhi vitendea kazi kwa Katibu wa  Bodi ya SHUWASA,Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA, Flaviana Kifizi wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga Mjini (SHUWASA). 
Wajumbe wa Bodi Mpya ya SHUWASA wakiwa na vitendea kazi vyao.
Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akipiga picha ya pamoja na Wajumbe wa bodi ya SHUWASA iliyomaliza muda wake.
Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akipiga picha ya pamoja na Wajumbe wapya wa  bodi ya SHUWASA.
Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akipiga picha ya pamoja na Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama.
Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akipiga picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Mamlaka mbalimbali za Maji nchini.
Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akipiga picha ya pamoja na Viongozi wa taasisi mbalimbali.
Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akipiga picha ya pamoja na viongozi wa dini.
Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wa SHUWASA.
Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wa SHUWASA.
Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wa SHUWASA.
Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wa SHUWASA.
Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wa SHUWASA.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527