Picha : WAZIRI WA MAJI ATEMBELEA NA KUKAGUA ENEO LA UJENZI WA MRADI WA MAJI MWAWAZA- SHINYANGA


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa ametembelea na kukagua eneo la ujenzi wa Mradi wa Maji kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga ambao utagharimu shilingi Bilioni 1.4 hadi kukamilika kwake.

Prof. Mbarawa ametembelea eneo la Mwawaza panapojengwa Tenki la Maji litakalogharimu shilingi milioni 100 na kuzungumza na wananchi wa kata ya Mwawaza leo Alhamis Januari 9,2020. 

Prof. Mbarawa alisema mradi huo unajengwa kwa usimamizi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Shinyanga SHUWASA na kuwataka wananchi wa Mwawaza kuchangamkia fursa kwa kushiriki katika ujenzi kwani watakuwa wanalipwa.

Prof. Mbarawa aliagiza mradi huo ambao tayari ujenzi wake wa Matenki umeanza ukamilike kufikia Machi mwaka 2020 ili kuondoa changamoto ya maji safi na salama ambayo imekuwa kero ya muda mrefu.

“Nataka mradi huu umalizike haraka matenki yajengwe ndani ya miezi miwili zoezi la kulaza mabomba lianze mara moja. Tunaleta mabomba yenye ubora kwa gharama nafuu hivyo wananchi mnapaswa kulinda miundo mbinu ya maji ili idumu”,aliongeza.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele aliishukuru serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli kwa kusikia kilio cha wananchi wa Mwawaza kuwapatia huduma ya maji safi na salama.

Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA, Flaviana Kifizi, alisema SHUWASA inasimamia na kujenga miradi ya maji kwa kutumia wataalamu wa ndani “Force account” katika wilaya za Shinyanga (Negezi – Mwawaza) na Kahama (Ngogwa – Kitwana) ambapo Miradi hiyo inahusisha ujenzi wa matenki na mtandao wa maji safi.

“Miradi hii inahusisha ujenzi wa matenki na mtandao wa maji safi. Hadi kufikia tarehe ya leo utekelezaji wa miradi hii upo katika hatua mbalimbali,ujenzi wa matenki umeanza na mafundi wapo site wakiandaa maeneo ambayo matenki hayatajengwa”,alisema Kifizi.

Alisema ulazaji wa mabomba unasubiri upatikanaji wa msamaha wa kodi ya ongezeko la thamani VAT ambao maombi tayari yamewasilishwa wizara ya fedha.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA,Flaviana Kifizi akimweleza jambo Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa (kulia) leo Alhamis Januari 9,2020 alipotembelea na kukagua eneo la ujenzi wa tenki la maji katika eneo la Mwawaza ikiwa ni sehemu ya Mradi wa Maji kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga ambao utagharimu shilingi Bilioni 1.4 hadi kukamilika kwake. Kushoto ni Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog.
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa akisisitiza kukamilika haraka ujenzi wa tenki la Maji katika kata ya Mwawaza ili wananchi waanze kupata huduma ya maji safi na salama.
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa akizungumza katika eneo la ujenzi wa tenki la maji. 
Eng. Christopher Shiganza akielezea kuhusu ujenzi wa tenki la maji katika kata ya Mwawaza.
Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele akiishukuru serikali kuwapatia maji wananchi wa Mwawaza.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi akiteta jambo na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa alipotembelea na kukagua eneo la ujenzi wa Mradi wa Maji kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga.
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wananchi wa Kata ya Mwawaza na kuwaeleza kuhusu mradi wa maji unaojengwa katika kata hiyo.
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa akiwahamasisha wananchi wa Mwawaza kushiriki katika mradi wa maji kwenye kata hiyo.
Wakazi wa Mwawaza wakimsikiliza Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa.
Wakazi wa Mwawaza wakimsikiliza Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa.
Wakazi wa Mwawaza wakimsikiliza Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa.
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela akizungumza katika kata ya Mwawaza wakati Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akiwaeleza wananchi kuhusu mradi wa maji unaojengwa katika kata ya Mwawaza.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele akizungumza katika kata ya Mwawaza wakati Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akiwaeleza wananchi kuhusu mradi wa maji unaojengwa katika kata ya Mwawaza.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Gulam Hafeez Mukadam akizungumza katika kata ya Mwawaza wakati Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akiwaeleza wananchi kuhusu mradi wa maji unaojengwa katika kata ya Mwawaza.
Diwani wa Kata ya Mwawaza Mhe. Juma Nkwabi akiomba wananchi wa Mwawaza washiriki katika mradi wa maji.
Mwananchi wa Mwawaza Catherine Francis akiishukuru serikali kwa kuwapatia huduma ya maji.
Mkuu wa shule ya Sekondari Mwawaza  Juliana Limbe akiishukuru serikali kwa kuwapatia huduma ya maji.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post