KASI YA MAAMBUKIZO YA KIRUSI CORONA YAONGEZEKA CHINA


Serikali kuu ya China imesema  kwamba idadi ya waathirika wa virusi vibaya kabisa vya Corona imeongezeka na kufikia 2,774 kote nchini humo, huku kukiwa na visa vipya 769 vilivyogundulika. 


Hata hivyo ilisema hakukua na taarifa mpya za vifo iliyothibitishwa tofauti na jimbo la Hubei, ambako mapema liliarifu watu 24 waliokufa kutokana na maambukizi ya virusi hivyo wanafanya idadi ya waliokufa hadi sasa kufikia 80.

 Rais wa China Xi Jinping ameuita mripuko huo kuwa ni hali ya wasiwasi mkubwa na kusema serikali ilikuwa inafanya juhudi za kuzuia safari na mikusanyiko ya umma wakati ikiwapeleka wahudumu wa afya na vifaa kwenye mji ambao ni kitovu cha janga hilo wa Wuhan.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527