HAWA NDIYO MABILIONEA WAPYA AFRIKA

Mtu tajiri zaidi barani Afrika Aliko Dangote

Mfanyabiashara Mohammed Dewji kutoka Tanzania ametajwa kuwa miongoni mwa mabilioni 20 wa Afrika katika ripoti ya jarida la Forbes la mwaka 2020.

Katika ripoti hiyo mfanyabiashara tajiri nchini Nigeria Aliko Dangote ameorodheshwa kwa mara ya tisa mfululizo, kuwa mtu tajiri barani Afrika .

Dangote mwenye umri wa miaka 62 ambaye anafanya biashara ya Simiti, Sukari na unga wa ngano ana utajiri wa dola Bilioni 10.1.

Dangote anafuatiwa na mfanyabiashara wa Misri Nassef Sawaris ambaye aliongeza utajiri wake kutoka dola bilioni 6.3 hadi dola bilioni nane.

Mfanyabiashara huyo anamiliki asilimia 5.7 katika kmapuni ya viatu ya Adidas . Ongezeko la hisa za Adidas liliomuongezea dola bilioni moja nukta tano katika akaunti yake.Bilionea kutoka Tanzania Mo Dewji

Bilionea aliyeorodheshwa katika nafasi ya tatu ni raia wa Nigeria Mike Adenuga ambaye utajiri wake unatokana na sekta ya mawasiliano na mafuta. Kampuni yake ya mawasiliano ya simu Globacom ndio ya tatu kwa ukubwa nchini Nigeria ikiwa na wateja milioni 43.

Alijipatia utajiri wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 26 akiuza kanda za viatu na vinywaji.

Bilionea aliyeorodheshwa wa nne barani Afrika ni mfanya biashara wa almasi na raia wa Afrika Kusini Nicky Oppenheimer.

Utajiri wa bilionea wa Tanzania Mo umedaiwa kupungua hadi dola bilioni 1.6.

Isabel dos Santos mwenye utajiri wa dola bilioni 2.2 amedaiwa kujipatia utajiri wake wakati babake alipokuwa rais ambapo alijipatia hisa katika makampuni mengi ya Angola pamoja na benki.

Mwanamke huyo ambaye ametajwa kuwa mwanamke tajiri zaidi barani Afrika amesema kwamba anamiliki hisa kutoka katika kampuni zilizopo Ureno, ikiwemo Telecom na runinga ya nyaya.

Msemaji wa Isabel aliambia jarida la Forbes kwamba ni mfanyabiashara huru .Mwana wa aliyekuwa rais wa Angola Isabel dos Santos ni miongoni mwa watu matajiri zaidi barani Afrika

Nicky ambaye ni mrithi wa mali ya familia yake ya Oppenheimer ana utajiri wa dola bilioni 7.7.

Familia yake imekuwa ikihusika na uuzaji wa almasi.
Orodha ya mbilionea 20 na utajiri wao barani Afrika:
  1. Aliko Dangote$10.1 B
  2. Nassef Sawiris$8 B
  3. Mike Adenuga$7.7 B
  4. Nicky Oppenheimer $7.7 B
  5. Johann Rupert $6.5 B
  6. Issad Rebrab $4.4 B
  7. Mohamed Mansour $3.3 B
  8. Abdulsamad Rabiu $3.1 B
  9. Naguib Sawiris$3 B
  10. Patrice Motsepe $2.6 B
  11. Koos Bekker$2.5 B
  12. Yasseen Mansour $2.3 B
  13. Isabel dos Santos $2.2 B
  14. Youssef Mansour $1.9 B
  15. Aziz Akhannouch $1.7 B
  16. Mohammed Dewji $1.6 B
  17. Othman Benjelloun $1.4 B
  18. Michiel Le Roux $1.3 B
  19. Strive Masiyiwa $1.1 B
  20. Folorunsho Alakija $1 B

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527