KAULI KANGI LUGOLA BAADA YA RAIS MAGUFULI KUMTUMBUA NA KUSEMA HAFAI


Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesema ataendelea kumsaidia Rais  Magufuli   kwa kuwa yeye ni mbunge wa Mwibara (CCM).

Lugola ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Januari 23, 2020  jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kumalizika hafla ya uzinduzi wa nyumba za  maofisa wa Jeshi la Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.

Alieleza hayo baada ya Rais  Magufuli  ambaye wakati akizungumza  katika uzinduzi huo kusema Lugola na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias  Andengenye hawafai kuendelea na nyadhifa zao kutokana na mambo waliyoyafanya kuhusu uingiaji wa mikataba.

“Rais ndiye aliniteua kwenye Baraza la Mawaziri na ndiye ameona anipumzishe, kwangu mimi ni jambo la faraja, Watanzania mmemsikia Rais hatua aliyochukua ni hatua nzuri na inalenga kujenga safu ya Serikali, ninaahidi kama Mbunge ambaye nilipata nafasi ya kumsaidia Rais nitaendelea kumsadia kwa kwa heshima kubwa." Amesema Lugola


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post