SEKTA YA MAWASILIANO YA SIMU INAVYOKUZA AJIRA NCHINI


Mwanzoni mwa mwezi huu wa Januari 2020, Naibu Waziri katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Atashasta Nditiye (Mb) alilitaka Shirika la Posta nchini (TPC)kujikita katika matumizi ya teknolojia na ubunifu katika utoaji wa huduma zake. Waziri Nditiye alienda mbali na kuelezea namna ambavyo mabadiliko ya kiteknolojia ya siku za karibuni yanavyosaidia kusukumu mbele ukuaji wa uchumi. 

Sekta ya mawasiliano ya simu ni moja ya sekta kubwa zaidi zinazosaidia kukua kwa uchumi wetu.Katika muongo mmoja uliopita sekta hiyo imewekeza kwa kiasi kikubwa kwenye teknolojia na kuwezesha ongezeko kubwa la watumiaji wa simu mpaka sasa kwa mamilioni. 

Sekta hiyo pia imekua kwa kiasi kikubwa kabisa. Matokeo ya ukuaji huo ni sekta hiyo kuweza kuajiri Watanzania zaidi ya milioni moja na nusu (1,500,000)katika maeneo ya wahandisi wa programu za kompyuta, huduma kwa wateja, uuzaji na usajili wa laini za simu na huduma za kutoa na kupokea fedha. Sekta hiyo inapoendelea kupanuka mfano kwenda katika mfumo wa 4G unaotoa huduma bora zaidi inaamaanisha pia itatengeneza ajira zaidi.

Wakati huo huo, kampuni nyingi za mawasiliano ya simu zinaendesha huduma ya kutuma, kupokea fedha na kulipia bili mbalimbali pamoja na huduma nyinginezo ambazo zimesaidia watu wengi kuingia katika mifumo rasmi ya kifedha na kukuza uzalishaji na biashara. Mfano mmojawapo ni kampuni ya Tigo.

Mbali na huduma hizo Tigo pia imesaidia kukua kwa biashara ndogo na za kati kwa kukuza uwezo wao kufanya mambo kidijitali ikiwemo kuunganisha mtandao wa intaneti katika maeneo ya biashara na ofisini.

Ama kwa hakika sote hatuna budi kuishukuru na kufurahia ukuaji wa sekta hii. Muungano wa siku za karibuni wa Tigo na Zantel katika kutoa huduma nao ni jambo jema kwani utaruhusu kampuni hizo kutoa huduma bora zaidi za pande zote mbili lakini kukuza faida ambayo itawekezwa kuboresha huduma zaidi na zaidi. 


Muungano wa aina hii ni aina mojawapo ya namna sekta hii inaweza kujengewa mazingira bora ya kukua. Tunapouanza mwaka mpya, ni vyema kama Taifa tukaendelea kuiunga mkono sekta hii kuhakikisha inaendelea kukua na kufaidisha wateja na uchumi wetu.Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post