ZIMAMOTO NA UOKOAJI WAENDELEA KUMTAFUTA MWANAFUNZI ALIYESOMBWA NA MAJI

Na John Walter-Babati

Mwili wa Mwanafunzi wa kiume (10) aliyekuwa akisoma darasa la nne katika shule ya Msingi Darajani iliyopo Mjini Babati mkoani Manyara  anayesadikiwa kusombwa na maji wakati akiogelea kwenye mto eneo linalojulikana kama  Darajani  unaotiririsha Maji kuelekea Ziwa Manyara bado haujapatikana kwa siku ya tatu sasa.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Manyara, Kamishna msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Julishaeli Mfinanga, amewataka wananchi wawe watulivu katika kipindi wanachoendelea na utafutaji.

Amesema mwelekeo wa kumpata mtoto huyo upo kwa sababu tabia ya maji huwa baada ya mtu kuzama kwenye kina kirefu cha  maji baada ya siku tatu humuibua juu na kumtupa kando ya mto.

Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya mji wa Babati,Viongozi wa serikali na Siasa wamejitokeza kwa wingi kusaidiana na vyombo vya ulinzi na Usalama katika kufanikisha zoezi la kuupata mwili wa mtoto huyo.

Hata hivyo  baaadhi ya wananchi wakizungumza na kituo hiki, wamesema kuwa kwa kipindi hiki cha mvua mto huu huwa unafurika maji mengi ambayo yana kasi kubwa, hivyo tahadhari inahitajika kwa wanaovuka katika eneo la mto huo pamoja na kuwa makini na watoto.

Mtoto huyo alisombwa na maji jumatatu Januari 20  majira ya saa saba mchana wakati wakiwa wanaogelea yeye na wenzake ambao walinusurika.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527