ZAIDI YA MIFUKO MBADALA 1400 ISIYOKUWA NA VIWANGO YAKAMATWA NJOMBE

Na Amiri Kilagalila-Njombe
Baraza la taifa la hifadhi ya mazingira NEMC kanda ya nyanda za juu kusini wamefanya oparesheni mjini Njombe na kukamata vifungashio zaidi ya 1400 visivyokidhi ubora wa soko katika maduka mbalimbali ya wafanyabiashara.


Katika oparesheni hiyo mifuko mbadala ambayo haina nembo ya ubora TBS na maelezo ya ubora wa mfuko pamoja na mifuko ya plastiki inayotumika kufungashia nyama mabuchani,karanga na hata mahindi ya kukaangwa imekamatwa .

Baadhi ya wafanyabiashara waliokamatwa akiwemo Afla Sanga na Anitha Mgaya, wamekiri kufahamu kuwa wamekiuka sheria na wengine wamedai kuwa  hawajui chochote kwa kuwa wengine sio wamiliki wa maduka bali ni wafanyakazi.

“Kwa mimi elimu hiyo sikuwa nayo,kwasabau unajikuta umeenda kununua mfuko wa kifungashio unafika pale unachukuwa mfuko unaoonekana sokoni na kuja kuuza”alisema Afla Sanga

Kwa niaba ya afisa mtendaji wa mtaa wa kwivaha uliopo mjini Njombe mjumbe wa mtaa huo  bwana Willy Kiswaga anasema sheria zichukue mkondo wake kwa kuwa mifuko hiyo ilishapigwa marufuku.

Milton Mponda ni afisa mazingira kutoka NEMC  kanda ya nyanda za juu kusini amesema zoezi la kukamata na kutaifisha mifuko hiyo ni endelevu huku akitoa wito kwa wafanyabiashara kujiepusha na uuzaji wa vifungashio feki kwa kuwa faini yake ni jela miezi mitatu au faini ya kuanzia shilingi laki moja hadi laki tano kutegemeana na wingi wa mzigo.

“Mpaka sasa tumekamata pisi sio chini ya 1500,mingi tumekamata kwasababu haiikidhi viwango,na ile iliyokidhi tumeacha tumeacha waendelee ktumia na ndio inayoruhusiwa kisheria”alisema Milton Mponda

Mponda amesema mfuko mbadala ni lazima uwe na taarifa za mzalishaji pamoja na nembo ya TBS kwa maana ya kukidhi viwango vya TBS VSM 70 pamoja na kuonyesha uwezo wa mfuko kubeba mzigo


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527