GONJWA LA AJABU LAIKUMBA CHINA


Mamlaka  ya China imeanzisha utafiti kuchunguza virusi vinavyosababisha ugonjwa wa ajabu ambao umewaambukiza watu kadhaa katika mji wa Wuhan.


Kesi za watu 44 zimeripotiwa na kuthibitishwa hadi sasa, visa 11 kati yake vinatajwa kuwa hatari zaidi, maofisa wamesema 

Mlipuko wa ugonjwa huo umefanya mji wa Singapore na Hong Kong kuanza kuchunguza watu wanaosafiri kutoka mji huyo.

Ugonjwa huo umezua hofu mtandaoni na kuhusisha virusi hivyo kuwa unaweza kusababisha kuwa na mtindio wa ubongo na madhara mengine yanayoweza sababisha vifo.

Uwezekano wa ugonjwa huo kufanana na ugonjwa wa ‘sars’ ambao uliua watu zaidi ya 700 ulimwenguni kote mwaka 2002-03, baada ya kutokea nchini China.

Kumekuwa na uvumi kwenye mitandao ya kijamii na kuhusisha ugonjwa huo kuwa unaambukiza kwa kasi sana.

Polisi wa Wuhan amesema kuwa watu wanane wameadhibiwa kwa kuchapisha taarifa za uongo katika mitandao bila ya kuwa na uhakika kuhusu ugonjwa huo.

Tume ya afya ya Wuhan imesema kuwa inafanya uchunguzi wa chanzo cha mlipuko wa ugonjwa huo.

Katika hotuba yake katika mtandao umesema kuwa tayari imeangazia vyanzo vya maambukizi ya ugonjwa huo na dalili zake lakini hotuba hiyo haikutaja kuwa unafanana na ugonjwa wa ‘Sars’ ambao uliwahi kusambaa duniani kote na kuua watu huku ukiwa umeanzia China.

Vilevile hakutaja iwapo kuna maambukizi ya kati ya binadamu na binadamu.

Hatua ya kuhusisha maambukizi hayo na soko la samaki, lilisababisha mamlaka kutaka kufanya usafi katika maeneo hayo.

Msemaji kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) amesema kuwa wana taarifa kuhusu ugonjwa huo na walikuwa wanawasiliana kwa karibu na Serikali ya China.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527