BUNGE IRAQ LAPIGA KURA KUWAFUKUZA WANAJESHI WA KIGENI BAADA YA MAREKANI KUMUUA JENERALI WA IRAN


Bunge la Iraq limepiga kura kupitisha azimio linaloitaka serikali kuviamrisha vikosi vya kijeshi vya kigeni kuondoa nchini humo. 

Hatua hiyo imechukuliwa katika kikao cha dharura kilichoitishwa leo. 

Azimio hilo hasa linalenga kumaliza makubaliano yaliyoafikiwa mika minne iliyopita yaliyoiruhusu Marekani kutuma vikosi vyake vya kijeshi kusaidia katika vita vya kupambana na kundi linalojiita Dola la Kiislam IS. 

Kura hiyo imepigwa siku mbili baada ya Marekani kumuua jenerali wa kijeshi wa Iran Qassem Soleiman akiwa nchini Iraq. 

Azimio hilo limeungwa mkono na wabunge wa madhehebu ya Kishia wenye mafungamano na Iran, ambao ndiyo wenye viti vingi bungeni. 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527