JAMBO YATAMBULISHA BIDHAA TATU MPYA “JAWIZA APPLE CRUSH SODA, JAMUKAYA JUISI YA UKWAJU NA UBUYU”

Jawiza Apple Crush  Soda
Jamukaya Ubuyu Juice
Jamukaya Ukwaju Juice

Na Moshi Ndugulile - Shinyanga 
Kampuni ya Jambo Food Products Limited iliyopo Mkoani Shinyanga imezindua bidhaa mpya ya Jawiza Apple Crush Soda,Juisi ya Ukwaju na Ubuyu zenye ujazo wa mili lita 300 ambazo zinapatikana kwa bei ya reja reja shilingi 500/= bei ambayo ni ya kizalendo kwa kila Mtanzania kwenye kipato cha kawaida. 

Bidhaa hizo tatu zenye ubora wa kimataifa zilizotengenezwa kwa ubora wa hali ya juu kwa kutumia teknolojia ya kisasa yenye mitambo kutoka Ujerumani zimetambulishwa rasmi leo Ijumaa Januari 10,2020.

Akizungumza wakati wa kutambulisha bidhaa hizo, Meneja masoko wa Kampuni ya Jambo Food Products Innocent Mafuru amesema Bidhaa mpya ya Apple Crush Soda ina ladha ya Apple inayotokana na matunda asili yanayopatikana hapa nchini Tanzania. 

“Jambo Food Products Limited tunayo furaha kuwatangazia wateja wetu nchi Nzima ujio rasmi wa wa bidhaa yetu mpya ya Apple Crush Soda. Apple Crush Soda ni kati ya bidhaa tulizonazo na kila mara tumeona ni vizuri kuwapa wateja wetu kitu kipya kulingana na mahitaji yao. 

Bidhaa ya Apple Crush Soda ina ujazo wa mili lita 300 na inapatikana nch nzima kwenye maduka yote ya jumla na reja reja kwa bei ya kizalendo ya shilingi 500/= pesa ya Kitanzania. Tumeweka bei hii ili kumfanya kila Mtanzania awe na uwezo wa kukata kiu na kuonja ladha tofauti kutoka kwetu”,ameeleza Mafuru.

Mafuru amesema mbali na kuzindua Apple Crush Soda pia wamezindua bidhaa nyingine mbili za Juisi zenye ladha ya Ukwaju na nyingine yenye ladha ya Ubuyu. 

“Bidhaa za Juisi ya Ukwaju na Ubuyu zote zina ujazo wa mili lita 300 na zinapatikana kwa bei ya reja reja shilingi 500/= bei ambayo ni ya Kizalendo kwa kila Mtanzania mwenye kipato cha kawaida”,ameongeza Mafuru. 

"Ubora wa bidhaa hizi ni wa kimataifa ,mchakato wa utengenezaji wake umechukua miezi nane mpaka kupata ubora huu.Bidhaa hizi ni salama na zina faida mbalimbali kiafya,ikiwemo Vitamini C na virutubisho mbalimbali katika kuupa mwili kinga”,amesema Mafuru. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jambo food Products Limited Salum Khamis amesema uwekezaji wa biashara zake umezingatia uzalendo kwa Watanzania na kwamba ni fursa kubwa katika utoaji wa ajira hasa kwa wazawa na kwamba kundi la wanawake linapewa kipaumbele zaidi. 

“Jambo Food Products tumeendelea kuwa wazalishaji wa vinywaji baridi vyenye ubora kwa kutumia teknolojia ya kisasa yenye mitambo kutoka Ujerumani na mwaka huu 2020 tumejipanga kuwafikia wateja wetu nchi nzima kwa kuongeza wasambazaji na mawakala nchi nzima ili kusogeza huduma zetu kwa kila Mtanzania”,ameeleza Khamis. 

“Tumekuwepo sokoni kwa muda wa miaka mitatu lakini kwa muda huo tumeweza kuwafikia wateja wengi hususani Kanda ya Ziwa na tunawashukuru wateja wetu kwa kutufanya kuwa chaguo lao namba moja”,amesema Khamis. 

Amewaomba wateja wao kuendelea kufurahia bidhaa zao mpya na wajivunie bidhaa zenye ubora wa kimataifa zilizotengenezwa nchini Tanzania kwa bei ya kizalendo.





Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527