Picha: AJALI YA BASI LA BRIGHT LINE,GARI NDOGO NA PIKIPIKI YAUA WATU WAWILI NA KUJERUHI 20 SHINYANGANa Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Watu wawili wamefariki dunia na wengine 20 kujeruhiwa baada ya gari lenye namba za usajili T.437 DFJ Yutoung Bus  Kampuni ya Bright Line iliyokuwa inatokea Mwanza kwende Dodoma kugongana uso kwa uso na gari lenye namba za usajili T.173 ANW Nissan Station Wagon wakati mwendesha  pikipiki yenye namba MC.489 BVR Sanlg akikwepa mwendesha baiskeli katika eneo la Isela barabara kuu ya Shinyanga kuelekea Tabora.


Ajali hiyo imetokea leo Jumatatu Januari 13,2020 majira ya saa nne asubuhi wakati basi hilo likitoka Mwanza kwenda Dodoma,gari ndogo ikitokea Tinde kuelekea Shinyanga na mwendesha pikipiki akitokea Shinyanga kuelekea Tinde.

Waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni mwendesha boda boda aliyejulikana kwa jina moja la Saidi na abiria aliyekuwa kwenye basi aliyejulikana kwa jina la Pilly Abed (12) mwanafunzi wa Dodoma.

Kwa Mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Joseph Paul chanzo cha ajali hiyo ni mwendesha pikipiki kumkwepa mwendesha baiskeli wakati akilipita basi la Bright Line bila kuchukua tahadhari.

Amesema majeruhi wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga na miili ya marehemu imefadhiwa katika chumba kuhifadhia maiti katika hospitali hiyo.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga,Rose Malisa amesema wamepokea miili ya marehemu wawili na majeruhi 20.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post