ADAIWA KUKUTWA NA MIHURI 56 YA SERIKALI IKITUMIKA KUGHUSHIA NYARAKA


Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia ABRAHAM  OBEDI [55] wakala wa bima ya GTM na Mkazi wa Isanga Jijini Mbeya akiwa na mihuri hamsini na sita [56] ya idara mbalimbali za serikali na ofisi binafsi ambayo imeghushiwa na kuhifadhiwa katika ofisi yake ya Stationaries.

Mtuhumiwa alikamatwa Disemba 31, 2019 majira ya saa 17:00 jioni huko maeneo ya Mtaa wa Sokoine uliopo Kata na Tarafa ya Sisimba Jijini Mbeya baada ya Jeshi la Polisi Mkoani hapa kupata taarifa na kisha kufanya msako mkali na kufanikiwa kumtia nguvuni mtuhumiwa pamoja na vielelezo.

Baadhi ya mihuri na nyaraka alizokutwa nazo mtuhumiwa ni kama ifuatavyo:-

1.Mhuri wa Mwenyekiti wa Mtaa wa Soko Kata ya Ruanda,

2.Mhuri wa Afisa biashara wa Halmashauri ya Mbeya,

3. Access Bank Tawi la Mbeya,

4.Mamlaka ya Mapato Mbeya [TRA]

5. Hakimu Mkazi Mahakama ya Mwanzo Mbeya Mjini,

Aidha mtuhumiwa alikutwa pia na  Kompyuta moja aina ya Accer, Stika za bima, Poss Machine na nyaraka mbalimbali vikiwemo vyeti vya wanafunzi ambao vimeghushiwa. Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

KUPATIKANA NA BHANGI.
Jeshi la Polisi Mkoani hapa linamshikilia AGREY MASHAKA @ MBOTO [25] Mkazi wa Kilambo Wilayani Kyela akiwa na dawa za kulevya aina ya bhangi kavu kilogramu thelathini [30].

Mtuhumiwa alikamatwa Disemba 31, 2019 majira ya saa 14:45 mchana baada ya Jeshi la Polisi Mkoani hapa kufanya msako mkali huko Kitongoji cha Kilambo, Kata ya Njisi, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela na Mkoa wa Mbeya. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa bangi hiyo. 

Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post