ACT -WAZALENDO YATANGAZA UCHAGUZI MKUU ILI KUPATA VIONGOZI WAPYA IKIWEMO NAFASI YA ZITTO KABWE


Chama cha ACT -Wazalendo nchini Tanzania kimefungua pazia kwa wanachama wake wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kuchukua fomu.


Nafasi zitakazogombewa ngazi ya Taifa ni kiongozi wa chama, naibu kiongozi, mwenyekiti wa Taifa, makamu mwenyekiti Taifa - Tanzania Bara na Zanzibar, katibu mkuu, wajumbe wa halmashuri kuu (nafasi 15) na wajumbe wa kamati kuu (nafasi nane)

Akizungumzia na waandishi wa habari jana Jumatatu Januari 27, 2020 katibu mkuu wa chama hicho,  Dorothy Semu amesema uchaguzi wa viongozi wakuu utafanyika Machi 14, 2020 ukitanguliwa na chaguzi nyingine za ngome ya wazee, ngome ya vijana na ngome ya wanawake.Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post