SERIKALI YAOMBWA KUANGALIA WAWEKEZAJI WAZAWA



Mchoro kwa ajili ya kuziba sehemu ya barabara iliyoharibika
Muonekano wa barabara iliyozibwa kwa kutumia lami ya baridi baada ya kuzibwa viraka maeneo yaliyoharibika.

Na Hellen Isdory Dar es Salaam.

Serikali nchini imetakiwa kutumia Viwanda vya wazawa wa ndani ili kuweza kukuza dhamira yake ya kuwainua wananchi wanyonge kiuchumi na kuboresha mazingira ya uwekezaji.

Na hii ni kwa kuangalia dhima kuu iliyokubaliwa na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo ni kuendelea kujenga uchumi wa Viwanda utakaochochea Ajira na Ustawi endelevu wa jamii.

Hayo yalibainishwa jana na Mkurugenzi wa Masoko toka Kampuni ya Kitanzania ya Starpeco jijini Dar es Salaam inayojishughulisha na uzalishaji wa Vialainishi Maalum na vya kawaida Jones Mkoka wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam namna teknolojia ya kisasa ya kutengeneza lami kwa kutumia maji badala ya mafuta inavyofanya kazi tofauti na ilivyozoeleka hapo awali ambapo teknolojia hiyo inatajwa kuwa ni rafiki wa mazingira.

Jones alisema kuwa teknolojia hiyo ndiyo inayotumika kwa sasa kwa nchi nyingi zilizoendelea na ina uwezo wa kuzalisha lita 15,000 kwa saa huku soko lake likiwa kubwa barani Afrika.

“Hii teknolojia ndiyo yenye soko kubwa ndani na nje ya nchi hivyo inatakiwa kuitazama kwa umakini na kama nchi kuweza kuitumia hasa kwa wakati huu ambapo serikali hii ya awamu ya Tano ilivyojikita katika kutengeneza miundombinu ya barabara lakini pia katika kukufua viwanda vya wazawa”,alisema Jones

Mkurugenzi huyo aliongeza kwa kusema kuwa teknolojia hiyo inatumia idadi ndogo ya wataalamu katika kuendesha mashine zake tofauti na ile ya awali ambayo lami ilikuwa ikichemshwa kwa kutumia kuni ambazo zinatokana na uharibifu wa mazingira.

“Teknolojia hii inaweza mkubwa wa kutunza mazingira kwani lami haichemshwi kama lami ya awali hivyo ikitumika itaweza kunza mazingira kwa kiasi kikubwa kwani ukizingatia kwasasa nchi ilivyojikita kutengeneza miundombinu ya barabara na pia ukizingatia tunahitaji miti yetu kuendelea kukua ili mvua inyeshe na wakulima walime”,aliongeza.

Aidha Jones alisema kampuni hiyo ipo sambamba na Juhudi za serikali hii ya awamu ya tano ya kufikia uchumi wa viwanda ambapo wameweza kushiriki miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara, madaraja, viwanja vya ndege hapa nchini.

“Ushiriki wetu kama Starpeco kwenye utekelezaji wa miradi hii upo kwa ushiriki wa moja kwa moja ambayo ni kuzalisha na kusambaza lami ya maji (Bitumen Emulsion) na lami ya mafuta (Cut backs) ambazo zinatumika kwenye utekelezaji wa miradi ya barabara,” alisema.

Hata hivyo alibainisha miradi mikubwa ambayo wame shiriki moja kwa moja kwa kusambaza lami na vilanishi mitambo hapa nchini ambayo ni mradi wa ujenzi wa daraja la Mfugale (TAZARA) kuanzia mwanzo mpaka mwisho, ujenzi wa barabara za juu kwenye makutano ya Ubungo, mradi wa upanuzi wa barabara ya Morogoro, upanuzi wa barabara ya Bagamoyo, uwanja wa ndege wa Tabora na Chato, ukarabati wa uwanja wa ndege wa KIA, mradi wa ujenzi wa jengo la tatu (Terminal Three) kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere na miradi mbalimbali ya barabara.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527