MAMLAKA YA DAWA NA VIFAA TIBA (TMDA) YAKABIDHI MSAADA WA DAWA NA TAULO ZA KIKE GEREZA LA SEGEREA


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Bw. Adam Fimbo atembelea gereza la Segerea na kutoa msaada wa caton 45 za taulo za kike, caton 10 za pampas na dawa mbalimbali kwa ajili ya wanahitaji ambao ni wafungwa na mahabusu wa gereza la Segerea.

Pichani ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (TMDA), Bw. Adam Fimbo akimkabidhi Mkuu wa Gereza la Segerea Afande George Wambura msaada wa katoni 45 za taulo za kike, katoni 10 za Pampas na dawa mbalimbali kwa ajili ya wanahitaji ambao ni wafungwa na mahabusu wa gereza la hilo jana jijini Dar es salaam Kulia ni Dkt. Benard Nyaongo wa Zahanati ya Gereza la Segerea na Kushoto ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo Ispekta Shukrani Rububula.
Mkuu wa Gereza la Segerea Afande George Wambura akimpongeza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Bw. Adam Fimbo mara baada ya kukabidhiwa msaada wa katoni 45 za taulo za kike, katoni 10 za Pampas na dawa mbalimbali kwa ajili ya wanahitaji ambao ni wafungwa na mahabusu wa gereza la hilo jijini Dar es salaam katikati ni Dkt. Benard Nyaongo wa Zahanati ya Gereza la Segerea na Kaimu Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo Inspekta Shukrani Rububula.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Bw. Adam Fimbo na Mkuu wa Gereza la Segerea Afande George Wambura wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya makabidhiano ya msaada huo Kulia ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo Ispekta Shukrani Rububula na kushoto ni Dkt. Benard Nyaongo wa Zahanati ya Gereza la Segerea.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Bw. Adam Fimbo na Mkuu wa Gereza la Segerea Afande George Wambura pamoja na Kaimu Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo Ispekta Shukrani Rububula wakijadiliana jambo mara baada ya kukabidhiana nyaraka zenye orodha ya dawa na vifaa vilivyotolewa kama msaada kwa zahanati hiyo katikati ni Dkt. Benard Nyaongo wa Zahanati ya Gereza la Segerea na kushoto ni Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma,wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA),Gaudensia Simwanza.
Mkuu wa Gereza la Segerea Afande George Wambura akitoa shukurani zake kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Bw. Adam Fimbo mara baada ya kukabidhiwa msaada huo kushoto ni Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma,wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA),Gaudensia Simwanza na katikati ni Dkt. Benard Nyaongo wa Zahanati ya Gereza la Segerea.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Bw. Adam Fimbo akipokea zawadi ya mkoba kutoka kwa Mkuu wa Gereza la Wanawake Segerea Afande Teopista Gauza wakati alipotembelea gereza hilo na kukabidhi msaada wa dawa na vifaa mbalimbali, Anayeshuhudia tukio hilo ni George Wambura Mkuu wa Gereza la Segerea. 
Msaada wa vifaa mbalimbali pamoja na dawa uliokabidhiwa kwa George Wambura Mkuu wa Gereza la Segerea na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA).
Mkuu wa Gereza la Segerea Afande George Wambura akitoa maelezo kwa kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Bw. Adam Fimbo wakati alipotembelea zahanati ya gereza hilo na kutoa msaada wa dawa na vifaa mbalimbali kwa ajili ya wafungwa.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Bw. Adam Fimbo akizungumza jambo na Mkuu wa Gereza la Segerea Afande George Wambura wakati alipotembelea zahanati hiyo na kujionea huduma mbalimbali za kitabibu zinavyofanyika.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Bw. Adam Fimbo akiongozwa na Mkuu wa Gereza la Segerea Afande George Wambura na Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo Ispekta Shukrani Rububula wakati akitembelea na kujionea huduma zinavyotolewa katika zahanati hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Bw. Adam Fimbo akiongozwa na Mkuu wa Gereza la Segerea Afande George Wambura wakiwasili katika zahanati hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527