BABA ALIYEKUTWA AKIWA UCHI NA MWANAYE KATIKATI YA MAPOROMOKO YA MAJI AKAMATWA MOROGORO

Kamanda wa Polisi mkoa wa morogoro, Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi Wilbroad Mutafungwa akiwaonyesha wanahabari(hawapo pichani ) panga na msumeno alivyokutwa navyo, bwana Benson Benard (31) aliyekutwa uchi wa Mnyama yeye na Mtoto wake katikati ya Maporomoko ya Maji eneo la Mlimani Nguzo Camp.

Na Farida Saidy Morogoro

Jeshi La Polisi Mkoa wa Morogoro Benson Benard (31) aliyekutwa uchi wa Mnyama yeye na Mtoto wake katikati ya Maporomoko ya Maji eneo la Mlimani Nguzo Camp ndani ya manispaa hiyo na alipoamuliwa kuondoka eneo hilo hatarishi akajirusha na kujizamisha kwenye Maji yaliyokuwa wakitiririka kwa kasi kabla ya kushikiliwa na Polisi. 

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa morogoro, Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi Wilbroad Mutafungwa Askari wake walipokea taarifa toka kwa raia mwema juu ya uwepo tukio hilo na baada ya kufika eneo la tukio ambapo ni eneo la chanzo cha maji wakamkuta mtuhumiwa akiwa na Mtoto wake , na katika hali ya kushangaza wote walikua uchi wa mnyama.

Aidha katika Eneo hilo la Tukio Askari Polisi walikuta Panga na Msumeno ambapo pia kunadaiwa kumefanyika uharibifu wa mabomba ya maji, na sasa mtuhumiwa anashikiliwa na Polisi kwa mahojiano.

Hata hivyo Mtoto amekabidhiwa kwa mama yake mzazi Mary Shao mkazi wa Kihonda, ambae nae anasema muwewe alianza kubadilika kwa kuongea mambo yasiyo eleweka na siku hiyo ya tukio aliaga anaenda kuogelea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post