MFUNGWA ALIYEKATAA KURUDI URAIANI KWA MSAMAHA WA RAIS ADAI HANA PA KWENDA'



Mfungwa Merald Abraham, aliyekataa kurudi Uraiani

Mfungwa mmoja aliyejulikana kwa jina la Merald Abraham, amekataa kurejea Uraiani baada ya kuachiwa kwa msamaha uliotolewa na Rais Magufuli kwa madai ya kuwa hana pa kwenda na kutaka ahamishiwe katika Gereza la Ukonga, Jijini Dar es Salaam.

Abraham ni miongoni mwa wafungwa 70 katika Gereza la Ruanda, waliopewa msamaha Desemba 9, 2019, na jana  Desemba 10 wakati wenzake wakiachiwa huru, yeye alikataa kubaki huru hali iliyopelekea kujijeruhi usoni, akishinikiza kuendelea kubaki mahabusu.

"Sina pa kwenda, bora nibaki Gerezani, ikiwezekana nitolewe hapa nihamishiwe Gereza la Ukonga Dar es Salaam, ila sio Uraiani" amesema Abraham.

Jana wakati wa Maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania, ambayo Kitaifa yalifanyika mkoani Mwanza, Rais Magufuli alitoa msamaha kwa wafungwa takribani 5,533 na wafungwa 259 kati yao wanatoka mkoani Mbeya.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527