Picha : TGNP YAKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI KUVUNA MATOKEO YA MAFUNZO YA USHIRIKI WA WANAWAKE KWENYE UONGOZI


Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP Mtandao) umeendesha warsha ya kuvuna matokeo kutoka kwa waandishi wa habari wa mikoa mbalimbali nchini waliopewa mafunzo juu ya ushiriki wa wanawake katika uongozi ikiwemo siasa. 


Warsha hiyo ya siku mbili imeanza leo Jumanne Desemba 17,2019 kwenye ukumbi wa mikutano wa Silver Paradise Hotel jijini Dar es salaam. 

Warsha hiyo imekutanisha waandishi wa habari kutoka mikoa ya Shinyanga,Rukwa,Kilimanjaro, Ruvuma,Pwani,Morogoro na Dar es salaam kwa ajili ya kuwajengea na kuongezea uelewa na uwezo wa kuripoti masuala ya kijinsia hasa katika kuhamasisha ushiriki wa wanawake na vijana kwenye uongozi. 

Afisa Habari wa TGNP Mtandao Monica John amesema lengo ni kuvuna matokeo yaliyotokana na mafunzo yaliyofanyika mwezi Septemba mwaka huu juu ya ushiriki wanawake katika uongozi. 

“Kupitia warsha hii washiriki wataelimishwa juu ya ilani ya uchaguzi ya wanawake na kuweka mikakati ya namna ya kuongeza kasi ya kuripoti masuala ya kijinsia kwenye vyombo vya habari hasa kusambaza ilani ya uchaguzi ya wanawake na kuhamasisha mila nzuri zinazohamasisha ushiriki wa wanawake na vijana katika uongozi”,ameeleza John. 

“Tutajadili changamoto,mafunzo na fursa zilizopo katika vyombo vya habari katika kuhamasisha jamii kuchagua na kuhamasisha wanawake kushiriki katika uongozi”,amesema John.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI

 Afisa Habari wa TGNP Mtandao Monica John akizungumza wakati wa warsha ya kuvuna matokeo kutoka kwa waandishi wa habari wa mikoa mbalimbali nchini waliopewa mafunzo juu ya ushiriki wa wanawake katika uongozi ikiwemo siasa leo Jumanne Desemba 17,2019 katika ukumbi wa Silver Paradise Hotel jijini Dar es salaam. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Afisa Habari wa TGNP Mtandao Monica John ambaye ni Mwezeshaji katika warsha hiyo akieleza namna waandishi wa habari wanavyoweza kutumia kalamu zao kuhamasisha mila nzuri zinazohamasisha ushiriki wa wanawake na vijana katika uongozi.
Afisa Habari wa TGNP Mtandao Monica John akizungumza kwenye warsha ya kuvuna matokeo kutoka kwa waandishi wa habari wa mikoa mbalimbali nchini waliopewa mafunzo juu ya ushiriki wa wanawake katika uongozi ikiwemo siasa.
Waandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania wakiwa ukumbini.
Waandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania wakiwa ukumbini.
Mwandishi wa habari wa Gazeti la Nipashe Marco Maduhu kutoka mkoa wa Shinyanga akitoa mrejesho wa kazi alizofanya baada ya kupewa mafunzo juu ya ushiriki wa wanawake katika uongozi ikiwemo siasa.
Mwandishi wa habari Bahati Nyakiraia kutoka mkoa wa Kilimanjaro akitoa mrejesho wa kazi alizofanya baada ya kupewa mafunzo juu ya ushiriki wa wanawake katika uongozi ikiwemo siasa.
Mackline Kamote wa Abood Media Morogoro akitoa mrejesho wa kazi alizofanya baada ya kupewa mafunzo juu ya ushiriki wa wanawake katika uongozi ikiwemo siasa.
Angel Mbalamwezi wa Nkasi Fm Rukwa akitoa mrejesho wa kazi alizofanya baada ya kupewa mafunzo juu ya ushiriki wa wanawake katika uongozi ikiwemo siasa.
Rodrick Mushi wa Star Tv mkoani Kilimanjaro akitoa mrejesho wa kazi alizofanya baada ya kupewa mafunzo juu ya ushiriki wa wanawake katika uongozi ikiwemo siasa.
Aden Mbelle wa Jogoo Fm mkoani Ruvuma akitoa mrejesho wa kazi alizofanya baada ya kupewa mafunzo juu ya ushiriki wa wanawake katika uongozi ikiwemo siasa.
Samuel Shao wa Radio Sauti ya Injili Moshi mkoani Kilimanjaro akitoa mrejesho wa kazi alizofanya baada ya kupewa mafunzo juu ya ushiriki wa wanawake katika uongozi ikiwemo siasa.
Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini.
Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini.
Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini.
Warsha inaendelea.
Warsha inaendelea.
Washiriki wa wasrha wakiwa katika kazi ya kundi.
Kazi ya kundi ikiendelea.
Kazi ya kundi ikiendelea.
Washiriki wa warsha wakijadili jambo ukumbini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527