MVUA YAZUA KIZAA ZAA DAR..MAJI KILA KONA


Mvua zilizoanza kunyesha leo asubuhi ya Disemba 17, 2019, jijini Dar es salaam, zimepeleeka mafuriko katika baadhi ya maeneo ya jiji hilo na kusababisha kadhia na kero mbalimbali kwa wananchi.

Kutokana na changamoto hiyo ya mvua vitu mbalimbali vimeonekana vikisombwa na maji hayo ikiwemo sofa huku watu mbalimbali wakijitolea kuwaokoa watoto kwa kuwavusha kutoka upande mmoja kwenda mwingine.

Mvua hiyo imetajwa kuathiri maeneo mengine ikiwemo : 

1. Jangwani Kutokea fire kwenda Magomeni na Magomeni kwenda fire. Imefungwa.

2. Jangwani kwa nyuma kutokea Kariakoo to kigogo imejaa Maji.

3. Umoja wa mataifa. Kutokea Almuntazir mpaka Muhimbili primary kumajaa Maji.

4. Scout upanga barabara ya malik pamejaa maji kuja junction ya Muhimbili

5. Barabara ya Fire hapa katika hospitali ya Regency pamejaa Maji

6. Kamata ktk barabara ya nyerere katika fly over ya treni pamejaa Maji

7. Kamata kutokea kariakoo kuja barabara ya nyerere pamejaa Maji.

8. Waterfront hapa kuja central police pamejaa Maji
  
9. Barabara ya Mwamnyange kuja main road ya barabara ya whitesand pamejaa Maji

10. Barabara ya Whitesand kuja round about ya whitesand  hali si shwari

11. Basihaya kuja Nyaishozi hali sio nzuri

12. Junction ya barabara ya gonna katika Mataa Maji yamejaa

13. Mbozi road Chang'ombe Maji  kuna maji ya kutosha

14. Junction ya hapa kwa sokota napo pamejaa Maji

15. Sinza Legho darajani hapa pamejaa maji pia

 16. karibu na ofisi za kiwango kuna daraja nalo limejaa maji ya kutosha litanata kutema kabisa, huko Mburahati, Kigogo ni mwendo wa mafuriko tuu maji yamejaa ndani, ukija hapo mkwajuni kwenye mto napo pamejaa maji yamepita mpaka barabara




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527