RAIS WA ZAMANI WA SUDAN, OMAR AL-BASHIR AHUKUMIWA MIAKA MIWILI JELA KWA RUSHWA | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, December 14, 2019

RAIS WA ZAMANI WA SUDAN, OMAR AL-BASHIR AHUKUMIWA MIAKA MIWILI JELA KWA RUSHWA

  Malunde       Saturday, December 14, 2019

Mahakama ya nchini Sudan imemkuta Rais wa zamani Omar al-Bashir na hatia ya makosa ya utakatishaji fedha na rushwa na kumhukumu kifungo cha miaka miwili gerezani. 


Hiyo ni hukumu ya kwanza katika msururu wa kesi zinazomkabili al-Bashir, ambaye pia anasakwa na mahakama ya Kimataifa ya Jinai – ICC kuhusiana na mashitaka ya uhalifu wa kivita na mauaji ya halaiki yanayohusiana na mgogoro wa Darfur katika miaka ya 2000. 

Hukumu ya leo inakuja ikiwa ni mwaka mmoja baada ya waaandamanaji nchini Sudan kuanzisha vuguvugu la mapinduzi dhidi ya serikali ya kimabavu ya al-Bashir. 

Wakati wa miongo yake mitatu madarakani, Sudan iliwekwa kwenye orodha ya Marekani kwa kufadhili ugaidi, na uchumi wa nchi hiyo ukasambaratishwa na miaka mingi ya usimamizi mbaya na vikwazo vya Marekani.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post